Naibu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade), Latifa Mohamed Hamis, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam.
Janeth Jovin na Tatu Mohamed
MAMLAKA ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) imesema kuwa jumla ya kampuni 2888 za hapa nchini na 43 kutoka nje zinatarajia kushiriki katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam yanayojulikana kama Sabasaba.
Akizungumza na waandishi wa habari leo katika viwanja vya maonesho vya Mwalimu Nyerere vilivyopo Kilwa Road Temeke jijini Dar es Salaam, Naibu Mkurugenzi wa Tantrade, Latifa Mohamed Hamis anasema mamlaka hiyo inawataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika maonesho hayo ili kujionea vitu mbalimbali kutoka kampuni za ndani na nje ya nchi zikiwamo za Uturuki, Silya, China na Misri.
Anasema wanafanya maonesho hayo chini ya muongozo wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambapo watachukua tahadhari katika kuwakinga washiriki na virusi vya corona.
"Safari hii maonesho haya yameanza tarehe moja Julai hadi 13 badala ya Juni 28 kama ilivyozoeleka, hali hii imetokana na changamoto ya virusi vya corona ila tunamshukuru Mungu kwa hapa kwetu Tanzania Mungu ametulinda na tukaona kuna haja ya kuyafanya maonesho ila kwa kuchukua tahadhari ambapo tumezingatia muongozo wa wizara ya afya.
Hivyo napenda kuwaambia wananchi wajitokeze kwa wingi kuja kuona mambo mazuri katika maonesho haya maana tumejipanga na kampuni hizi za ndani na nje zimejipanga na zina bidhaa na vitu vizuri," anasema
Aidha alisema kwa mwaka huu mikutano ya ana kwa ana ya biashara itafanyika kwa njia ya mtandao wa zoom hivyo washiriki watapata fursa ya kukutana na kubadirishana mawazo na inatarajia kufanyika kuanzia Julai 2 hadi 6 , mwaka huu.
"Kupitia mikutano hii washiriki ambao wapo nyumbani wataweza kushiriki na hapa tumewalenga wale wateja wetu kwa sababu ya changamoto ya corona hawakuweza kuja lakini watapata fursa ya kushiriki kwa njia ya mtandao wa zoom," anasema
Hata hivyo anasema katika maonesho hayo wasanii wa filamu, muziki na vishekesho ambao ni wajasiliamali wabunifu watapata fursa ya kuonesha bidhaa zao.
"Tutakuwa na kijiji cha masupastaa, ndani ya hicho kijiji watu watakutana na wasanii wengi wajasiliamali ambapo pamoja na kuwaona mubashara pia watapata fursa ya kununua bidhaa zao," anasema

No comments:
Post a Comment