HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 02, 2020

WAZIRI MKUU MAJALIWA MGENI RASMI SIKU YA UZINDUZI WA MAONESHO YA SABASABA

Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa, akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), kuhusu maonyesho ya Kimataifa ya Sabasaba yatakayofunguliwa Julai 3, 2020 na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. (Picha na Francis Dande).
 Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa, akitembelea baadhi ya mabanda katika Maonyesho ya Sabasaba.




Na Janeth Jovin

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa anatarajia  kuwa mgeni rasmi katika Uzinduzi wa maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ambayo yanafanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere  maarufu kama Sabasaba.

Maonyesho hayo yalianza Julai mosi mwaka huu na kutarajia kuisha julai 13 mwaka huu.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa, amesema  licha ya  nchi awali kukumbwa na ugonjwa wa Covid -19 unaosababishwa na virusi vya Corona ila mwitikio wa washiriki katika maonyesho hayo ni makubwa ukilinganisha na miaka ya nyuma.

Amesema jumla ya washiriki 2880 kutoka kampuni mbali mbali wanashiriki katika maonyesho hayo huku kwa makampuni ya nje yakiwa 43.

"Kwa  safari hii ushiriki umekuwa mkubwa licha ya nchi kukubwa na corona kipindi cha nyuma ila watu wamejitokeza kushiriki maonyesho haya ....tahadhari ya ugonjwa huu tumeizingatia kwa kuweka vitakasa mikono kila banda," amesema

Aidha amesema kupitia maonyesho haya watanzania wanapaswa kupenda bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi.

"Ili tuzidi kupanda katika Uchumi wa juu,kama juzi   Tanzania ilivyotangazwaa na Benki Kuu ya Dunia kuwa tumefika katika Uchumi wa kati tunapaswa kuongeza jitihada kupenda na kuthamini vitu vya ndani ya nchi na kufanya uchumi wa viwanda nchini kuwa endelevu,"amesema

No comments:

Post a Comment

Pages