Na Bebi Kapenya, Kilimanjaro
Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), umeendelea kurejesha mawasiliano
katika maeneo mbalimbali nchini yaliyoathiriwa na mvua zilizosababisha
athari kubwa kwa watumiaji wa barabara pamoja na madaraja.
Wakala
umejenga daraja la muda la Chuma la Mto Rau Halmashauri ya Wilaya ya
Moshi mkoani Kilimanjaro baada ya daraja la awali linalounganisha
Halmashauri ya Wilaya ya Moshi na Manispaa ya Moshi kuvunjika na
kusababisha kukosekana kwa mawasiliano kwa wananchi wa maeneo hayo.
Meneja
wa TARURA Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Mhandisi Roy Johansen alisema
baada ya kupata changamoto ya kuvunjika kwa daraja la mto Rau, Wakala
ulichukua hatua za haraka za kurudisha mawasiliano kwa kutengeneza
daraja la muda la Chuma lenye urefu wa mita 23 ili wananchi waweze
kuendelea na shughuli zao za kiuchumi kwani eneo hilo linahudumia Kata 2
zenye jumla ya vijiji 9.
”Sisi
kama Wakala tuliamua kutengeneza daraja la muda la Chuma kwa ajili ya
wapita kwa miguu, pikipiki na bajaji ili kurudisha mawasiliano kwa
wananchi kabla ya kutengeneza daraja jipya la kudumu, pia niwaombe
wananchi wa maeneo haya wawe na uvumilivu kwani tutajitahidi kadri ya
uwezo wetu ili mawasiliano ya awali yaweze kurudi”, alisema Meneja huyo.
Meneja
alisema hatua itakayofuata ni kutengeneza daraja la kudumu ambapo
tayari kwa kushirikiana na Ofisi ya Mratibu wa TARURA Mkoa wa
Kilimanjaro jumla ya fedha kiasi cha shilingi milioni 650 zimeombwa
TARURA Makao Makuu na tatizo hilo limeanza kushughulikiwa.
Aidha, Mhandisi Roy Johansen alisema, Wakala
umetafuta ufumbuzi mwingine wa changamoto inayowakabili wananchi wa
maeneo hayo kwa kuanza kutengeneza barabara ya Mandela Access iliyopo
upande wa pili wa maeneo hayo yenye urefu wa Km 4 ambapo barabara hiyo
itasaidia wananchi kusafirisha bidhaa zao kwa magari huku wakingojea
kutengenezwa kwa daraja la kudumu.
Naye,
Bw. Emmanuel Massawemkazi wa Kijiji cha Mamboleo ameishukuru Serikali
kwa kutengeneza kivuko hiko cha muda na kusema kimewasaidia sana kutatua
baadhi ya changamoto zilizokuwa zinawakabili na ameiomba Serikali
kupitia TARURA kuwajengea daraja kubwa ili magari yaanze kupita kama
hapo awali.
TARURA
inaendelea kurejesha mawasiliano katika maeneo mbalimbali nchini baada
ya mvua kunyesha kwa muda mrefu na kusababisha baadhi ya maeneo
kutopitika.
No comments:
Post a Comment