UTT
AMIS leo imefungua rasmi kituo cha
kuhudumia wawekezaji wetu katika jiji la Arusha.
Hii ni katika kutekeleza azma
yetu ya kuendelea kuwahudumia kwa karibu
zaidi wawekezaji wetu na kuwapatia huduma itakayovuka matarajio yao katika
uwekezaji.
Kupitia
kituo hichi tunatarajia wawekezaji wetu watapata
huduma mbalimbali ikiwemo, Ushauri na elimu ya uwekezaji kwenye mifuko ya
uwekezaji wa pamoja, kufungua akaunti, kuuza na kununua vipande,kupata taarifa za uwekezaji ,kujua thamani ya vipande katika
mifuko na huduma nyinginezo za uwekezaji.
UTT AMIS ni kampuni ya serikali inayohusika na uanzishaji na
uwendeshaji wa mifuko ya uwekezaji wa pamoja. Pia tunatoa huduma za usimamizi
wa mitaji binafsi (Wealth Management Services) UTT AMIS inatekeleza majukumu
yake kulingana na sheria ya Masoko ya Mitaji na Dhamana ya mwaka 1994 na
marekebisho yake pamoja na kanuni za mifuko ya uwekezaji wa pamoja za mwaka
1997. UTT AMIS kwa sasa inasimamia mifuko sita ya uwekezaji ambayo ni Umoja,
Wekeza Maisha, Watoto, Jikimu, Ukwasi na Bond Fund.
Kwa Kuwekeza katika mifuko ya uwekezaji,
wawekezaji wananufaika na unafuu wa
gharama za uwekezaji, utaalamu wa uendeshaji kupitia meneja wa mfuko. Pia
wawekezaji wanauwezo wa kufuatilia uwekezaji wao na kujua hali ya uwekezaji wao
na soko kwa ujumla kwa urahisi kwani thamani ya vipande vya mifuko hutolewa
kila siku ya kazi. Vilevile mifuko hufanya uwekezaji mseto katika dhamana
mbalimbali sawa na sera ya uwekezaji ili kupunguza hatari za uwekezaji na
kupata faida shindani.
Mifuko hii imeandaliwa ili kukidhi mahitaji ya wawekezaji
wadogo na wakubwa huku tukizingatia malengo yao, muda wa kuwekeza, ukwasi,uwezo
wa kuhimili changamoto uwekezaji na
usalama.
Mathalani mfuko wa Umoja kiwango cha kuanza
kuwekeza ni vipande 10 tu, sawa na wastani wa shilingi 6500. Mfuko wa Wekeza
Maisha unatoa faida pacha za uwekezaji na bima ya maisha kwa kiwango cha chini cha shilingi 8340 iwapo
mwekezaji atachagua mpango wa kuwekeza kila mwezi.
Mfuko wa watoto unalenga kuwawezesha wazazi
kuanza kuwekeza mapema ili kukidhi mahitaji ya elimu ya watoto wao.Kiwango cha
chini cha kuanza kuwekeza ni shilingi 10,000 tu. Mfuko wa Kujikimu unalengo la
kukuza mtaji na kutoa gawio kila robo mwaka au kwa mwaka mara moja. Mpango wa
robo mwaka kima cha chini cha kuwekeza ni shilingi milioni mbili(2,000,000/-)
tu na mpango wa mwaka kima cha chini cha kuanza kuwekeza ni shilingi milioni
moja (1,000,000/-) tu.
Mfuko wa Ukwasi unalenga wawekezaji wa muda
mfupi hadi mrefu wanaozingatia hatari ndogo za uwekezaji na urahisi wa ukwasi.
Kiwango cha chini ca kuanza kuwekeza ni
shilingi laki moja (100,000/-) na kiwango cha chini cha nyongeza ni
shilingi elfu kumi (10,000/) tu. Pia Mfuko wa Hatifungani (Bond Fund) unawekeza
zaidi katika dhamana za serikali.
Mfuko una mpango wa kukuza mtaji na mpango wa
gawio.
Mpango wa kukuza mtaji kiwango cha chini kuanza kuwekeza ni shilingi
elfu hamsini(50,000/-) na mpango wa gawio kila mwezi kiwango cha chini kuanza
kuwekeza ni shilingi milioni kumi(10,000,000) na gawio kila baada ya miezi sita
kiwango cha chini kuanza kuwekeza ni shilingi milioni tano(5,000,000/-) tu.
Pamoja na kuwa na mifuko hii ya uwekezaji, UTT
AMIS inatoa huduma binafsi ya usimamizi wa mitaji kwa mtu mmoja mmoja na kwa
taasisi. Kupita huduma hii tunasikiliza hitaji mahsusi la mwekezaji na
kumtengenezea mpango binafsi wa uwekezaji utakokidhi mahitaji yake. Kiwango cha
chini cha kuanza kuwekeza katika mpango huu ni shilingi milioni mia
moja(100,000,000/-) tu.
Ukubwa
wa rasimali za mifuko na faida
ipatikanayo katika mifuko ni miongoni mwa vigezo katika kupima utendaji na
ufanisi wa kampuni za uwekezaji. UTT
AMIS imeendelea kutoa elimu ya uwekazaji na uelewa unaendelea kuongezeka .Hadi
kufikia Juni 30, 2020 jumla ya mali
katika mifuko ni zaidi ya bilioni 400. Pamoja na changamoto katika soko la hisa,
thamani ya mifuko chini ya usimamizi wa UTT AMIS imeendelea kukua na kutoa faida shindani kwa wawekezaji na
kuendana na maendeleo ya soko kwa ujumla.
Pamoja
na kufungua kituo hiki, UTT AMIS imeendelea kuwekeza katika mifumo ya tehama
ili kuwezesha wawekezaji kuwekeza na kupata taarifa za uwekezaji kwa njia ya simu. Mifumo hii inafanya kazi kwa
mwekezaji kupiga * 150*82# na kisha kufuata maelekezo. Pia kwa kuanzia mifumo
ya UTT AMIS imeunganishwa na Mifumo ya benki ya CRDB ambayo pia ni msimamizi wa
mifuko. Hivyo, mwekezaji anaweza kununua vipande moja kwa moja kwa kutumia mifumo yote ya malipo ya benki ya
CRDB.
Hivyo
tunawakaribisha wananchi wa Arusha na maeneo ya jirani wafike na kutumia kituo
hichi kupata huduma zetu na kuwekeza kwenye mifuko ili kutunza na kukuza mitaji
yao.
UTT AMIS –
Mshirika hakika katika Uwekezaji
No comments:
Post a Comment