Mmoja wa mashuhuda katika droo ya kumpata mshindi wa gari akichanganya kuponi na kisha kuchagua moja ambayo ilimuibua Didas Marik mshindi wa gari.[/caption]
HATIMAYE mkazi wa Dar es Salaam, Didas Marik (42), Julai 1, 2020 amefanikiwa kuibuka mshindi wa zawadi kubwa ya gari aina ya Toyota FunCargo katika droo kubwa ya Bahati Nasibu ya Jishindie Gari iliyochezeshwa na Kampuni ya Global Publishers katika Viwanja vya Mabibo Sokoni jijini Dar na kuhudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Bahati Nasibu, Elibariki Sengasenga.
Bahati nasibu hiyo iliyokuwa ikiendeshwa kupitia magazeti namba moja ya michezo Tanzania kutoka Global Publishers, Spoti Xtra na Championi, ilidumu kwa takribani miezi mitatu ambapo ilizinduliwa Februari 27, mwaka huu na kuhitimishwa jana Julai Mosi, 2020.
[caption id="attachment_365656" align="alignnone" width="800"] Kuponi ya mshindi.[/caption]
Lengo la kuwepo kwa bahati nasibu hiyo ni kurudisha kidogo kinachopatikana kwa jamii ambayo imekuwa ikiyasapoti magazeti ya michezo ya Global Publishers kwa kwa zaidi ya miaka 20.
Kuponi ambayo imetoa mshindi ni ya Gazeti la Championi Ijumaa lililotoka Juni 12, mwaka huu ambapo mshindi huyo alitangazwa na Mtangazaji wa +255 Global Radio, Gabby Mtanzania, ambaye alizungumza naye moja kwa moja kwa njia ya simu.
[caption id="attachment_365654" align="alignnone" width="800"] Mtangazaji wa +255Global Radio, Gabriel Stephen akimtangaza mshindi wa gari baada ya kuponi yake kuibuka kidedea. [/caption]
Akizungumza baada ya kutangazwa kuwa mshindi, Didas alisema: “Kwanza nashukuru, siamini kama leo hii mimi ndiyo mshindi kwani ni kitu ambacho sijawahi kukipata kwa maana ya kwamba sijamiliki gari ingawa nilikuwa na ndoto hizo siku moja. Leo hii nimekuwa mshindi na naenda kumiliki gari langu.
“Mwanzo wakati bahati nasibu hii inaanza, sikuwa naamini kama ni kweli, lakini hivi sasa nimeamini moja kwa moja kwamba Global Publishers ni waaminifu na wa kweli.
[caption id="attachment_365655" align="alignnone" width="800"] Gabriel Stephen (kushoto) akimtaka msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Elibariki Sengasenga, aeleze machache baada ya kushuhudia bahati nasibu hiyo ilivyochezeshwa kwa uwazi.[/caption]
“Mimi ni msomaji mzuri wa magazeti ya Global hasa ya michezo ambayo ni Spoti Xtra na Championi, nawaambia wenzangu wasome haya magazeti kwani yanaandika habari za kweli na za uhakika kabisa. Hakuna janjajanja.”
Kabla ya kumpata mshindi wa droo hiyo kubwa, zilichezeshwa droo ndogo paopo hapo na kupatikana washindi sita waliojishindia Sh 50,000 kila mmoja.
[caption id="attachment_365651" align="alignnone" width="800"] Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Usambazaji, Anthony Adam, akiwashukuru wasomaji wote walioshiriki Bahati Nasibu hiyo na kuwaomba wazidi kujisomea magazeti ya Global Publishers kwa habari za uhakika. [/caption]
Washindi hao wa droo ndogo zilizochezeshwa ni Khalifa Mwipala, Seleman Ally Ruzegea, Maulid Ally, Msafiri Mawila ambao wote ni wakazi wa Dar. Wengine ni Mpoki Mwakyusa wa Mbeya na Kihiyo Hamisi kutoka Tanga.
Kabla ya kufanyika kwa droo hiyo, jana mapema kikosi cha Idara ya Usambazaji ya Global Publishers chini ya mkuu wake, Anthony Adam, kilizunguka mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar kuinadi bahati nasibu hiyo.
[caption id="attachment_365657" align="alignnone" width="800"] Mashabiki wa burudani wakinogesha mambo kwa kuimba na kucheza singeli muda mfupi kabla ya kumpata mshindi. Baadhi ya maeneo waliyozunguka ni Kimara, Mbezi, Mwenge, Ubungo na Mabibo.
Akizungumza baada ya mshindi kupatikana, Anthony alisema: “Tunawapongeza wote walioshiriki bahati nasibu hii. Siku zote mshindi huwa ni mmoja, hivyo kwa mliokosa msivunjike moyo kushiriki bahati nasibu zingine ambazo tutazianzisha.
[caption id="attachment_365652" align="alignnone" width="712"]
Mmoja wa mashuhuda akisoma kuponi yenye jina la mshindi wa shilingi elfu hamsini.[/caption]
“Lakini pia tuwafahamishe kuwa, mshindi atakabidhiwa zawadi yake ya gari katika ofisi zetu za Global Publishers siku ambayo tutaitangaza hapo baadaye.”
Ikumbukwe kuwa, tangu kuanzishwa kwa bahati nasibu hiyo, zilichezeshwa droo ndogo tatu ambapo zilitoa washindi 15 waliojishindia zawadi mbalimbali ikiwemo simu janja na wengine kuondoka na kitita cha fedha Sh 50,000.
(Stori: Marco Mzumbe | Picha na Richard Bukos | GPL)
No comments:
Post a Comment