Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Maonyesho
ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam , Barabara ya Kilwa
jijini Dar es salaam, Julai 3, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
NA TATU MOHAMED
WAZIRI
Mkuu Kassim Majaliwa amesema janga la ugonjwa wa Corona imeipa funzo
serikali kuimarisha sekta muhimu ikiwemo kilimo ili kuzalisha chakula
cha kutosha na cha ziada katika masoko.
Waziri
Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Julai 3, 2020 wakati akifungua Maonyesho
ya 44 ya Kimataifa ya Biashara (sabasaba), ambapo amesema kuwa serikali
imejidhatiti kuweka mazingira mazuri ya biashara na kuboresha masoko ya
bidhaa za ndani na kuvutia wawekezaji ili kukuza uchumi
"Tunatambua
mchango wa sekta binafsi, viwanda, kilimo na washiriki wa mnyororo wa
thamani na wataalamu walioshiriki katika maonyesho haya katika kukuza
uchumi," amesema.
Ameongeza
kuwa maonyesho hayo yatachochea kubadilishana uzoefu katika sekta ya
baishara na kuendelea kuhamasisha ukuaji wa uchumi wa kati.
"Pamoja na kuwapo kwa janga la Corona maonyesho haya yamefana na sekta ya viwanda na biashara zinaendelea kuimarika. Natambua
kuna mikutano ya ana kwa ana katika maonyesho haya, ambayo yatawajengea
uwezo washiriki, kupanua wigo wa masoko na fursa kwa wafanyabiashara,"
amesema.
Pia Waziri Majaliwa, ametoa wito kwa wazalishaji wa mazao kutafuta masoko ya uhakika.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania
(TanTrade), Dk Ng’wanza Kamata amesema baada ya kuambiwa muda mchache juu
ya uwepo wa Maonesho nayo waliweza kujipanga na kuhakikisha maandalizi
yanaenda vizuri
"Kutokana
ugonjwa huu wa Corona hata sisi tulikuwa tumehisi kuwa maonyesho haya
hayatakuwepo hadi pale ambapo tuliambiwa yatakuwepo na tulikuwa na muda
mchache wa maandalizi na tumeweza kufanya hiki tulichokifanya,” amesema
na kuongeza
" Kwa
mwaka huu washiriki waliohudhuria sio wengi sana ukilinganisha na mwaka
Jana hususani Kampuni za nje na tunajua sababu ambazo zimefanya
zisishiriki," amesema.
No comments:
Post a Comment