HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 02, 2020

Zaina Foundation Yawawezesha Wanahabari

Na Mwandishi Wetu
MKURUGENZI Mtendaji wa taasisi ya Zaina Foundation, Zaituni Njovu, amesema kuwa ni muhimu kwa waandishi wa habari kufahamu matumizi sahihi ya mtandao, na ulinzi Madhubuti wa taarifa na nyaraka zinazohifadhiwa mitandaoni

Akizungumza katika warsha ya siku moja iliyofanyika jijini Dar es Salaam iliyolenga kutoa mafunzo kuhusu matumizi ya huduma za mitandao na usalama mitandaoni iliyowahusisha waaandishi wa habari wanawake. Mkurugenzi huyo amesema kuwa watu wengi wanamiliki simu janja lakini hawana elimu ya kutosha kuhusu matumizi yake na usalama wao hususani wanapotumia huduma za mitandao

“Changamoto zaidi ipo kwenye suala zima la elimu watu wengi wanamiki simu Janja lakini hawana elimu juu ya matumizi sahihi ya mitandao na namna ya kujihakikishia usalama wa taarufa wanazohifadhi kwenye mfumo ya dijitali na mitandaoni. Hivyo tumeanza kutoa mafunzo hata kwa wanahabari hasa wanawake kwa sababu hii ni tasnia pekee ambayo ni makusudi kwaajili ya kusambaza taarifa kwa umma” Amesema Njovu

Ameongeza kuwa taasisi hiyo itahakikisha kuwa inatoa elimu kwa wananchi hususani katika uhifadhi wa taarifa na kuzilinda taarifa zilizohifadhiwa zisiweze kupotea au kudukuliwa.

“Sasa tunajifunza jinsi ya kuhifadhi taarufa hizi vizur kwenye intanet kupitia simu au kompyuta zao lakini pia tunajifunza jinsi ya kuzilinda ili zisipotee ama kudukuliwa, na hata zikipotea tunawaekeza mbinu pia za kuweza kuzirudisha (back up) ili basi jamii iendelee kunufaika kwa kupata taarifa kutoka kwa waandishi wa habari” Amesema Njovu.

Rahma salum ni miongoni mwa waandishi wa habari waliopata fursa ya kupoke mafunzo hayo na anasema kuwa amenufaika na mafunzo hayo kwa kujifunza jinsi ya kulinda taarifa zake zinaohusisha mitandao na dijitali kwa jumla.

“Leo ndo nimegundua kuwa teknolojia sio safe, hapo mwanzo nilikua nikifikiri kuwa maisha ya teknolojia ndio yananiweka safe(salama) zaidi na kuwa huru lakini kumbe sivyo!! Kupitia warsha hii nimejifunza umuhimu wa kuweka vitu vyangu mitandaoni private na kuchagua nini naweza kuhusu kila mtu aone na nini naweza fanya iki baadhi ya watu wasione.”amesema Rahm Salum

Zahara Tunda mwanahabari wa kujitegemea naye pia anaeleza namna alivyoyapokea mafunzo hayo

“Kupitia mafunzo hata nashukuru nmeweza kujua jinsi ya kutumia “signal” nilikua naskia tu signal na nilikua naona pia kwa watu ila nilikua sijui inatumikaje nashukuru sana leo nmeweza kujifunza kitu kipya katika mambo ya teknolojia.” Amesema Tunda

Matumizi ya Huduma za mtandao yanazidi kushika kasi duniani, na hii huchagizwa na maendeleo na kukua kwa teknolojia. Lakini pia uwepo wa mitandao ya kijamii.

Mpaka sasa Watu billion 4 .57 kwa mwaka 2020 ambayo mi sawa na asilimia 59% ya idadi ya watu duniani kote hutumia huduma za mitandao Watumiaji wa huduma za mtandao nchini Tanzania ni takribani million 2 laki saba na elfu hamsini ambayo ni sawa na asilimia 5.3 ya idadi ya watu wote nchini.

Zaina foundation ni taasisi isiyo ya kiserikali inayojihusisha na mkomboa mwanamke katika ufahamu wa masuala ya teknolijia na matumizi sahihi ya mtandao Hii itawasaidia wao kuwa salama katika kutuma nyaraka zao kama wanahabari lakini pia kuwasaidia kujishusha na udukuzi wa taarifa zao.

No comments:

Post a Comment

Pages