Lissu amesema kauli hiyo ni ‘Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watanzania’.
Lissu
ameyaeleza hayo jana akiwa Jimbo la Kawe ikiwa ni muendelezo wa chama
hicho kuzindua kampeni katika jiji la Dar es Salaam lwa siku tatu
mfululixo.
Lissu akowa jimboni hapo amesema, chochote kilichopo kwenye ilani ya chama chao kinabeba msingi wa kauli mbiu hizo..
Amesema
ilani yao ya Uchaguzi Mkuu huu ina kauli mbiu yenye maneno yafuatayo
ambayo ni Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu’, na kuongeza kuwa chochote
ambacho wamekisema katika ilani hiyo msingi wake ni uhuru wa watu na
maendeleo ya watu.
“Maendeleo tunayoyataka ni yanayozingatia
uhuru wa watu, yanayozingatia haki zao, maendeleo aliyoyaita Baba wa
Taifa maendeleo ya watu badala ya vitu” amesema Lissu.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEieZfRXIquGjYPENq0eA32KgcV5Acew9TsPMfQyAiBGG7Z5IX-sX1izrquebx7CyG29CaUSDhjQcwdMcyZbvoB52D4rCVb-0N3itz-E_AfqX5zcXrnWYOhYO6m6PdegIW985EN5KKoaWic/s640/Lissu.jpg)
No comments:
Post a Comment