Mwakilishi wa mkuu wa wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera Jovin Rutainurwa akizunguza na wadau wa sekta ya maji.
Sehemu ya wenyeviti wa vijiji na watendaji wa kata.
Na Lydia Lugakila, Kagera
Kamati za maji katika halmashauri ya wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera zimetakiwa kuwa wazi kwa wananchi juu ya miradi inayoletwa katika maeneo yao.
Kauli hiyo imetolewa na Antidius Augustine ambaye ni Mwenyekiti wa Shirika lisilo la kiserikali la Faraja For Hope and Organisation FAHODE katika mdahalo na wadau wa sekta ya maji uliyofanyika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera uliolenga kijadili suala la uwajibikaji wa huduma bora za jamii na kuona namna ya kuondokana na changamoto ya utelekezaji wa miradi ya maji katika vijiji vyao.
Augustine amesema kuwa wao kama Faraja wamekuwa wakitoa elimu mbalimbali kwa wananchi ili kuelewa, kujali na kutunza vyanzo vya maji.
Amesema kuwa ili heshima ya miradi iendelee kuheshimiwa na kutunza kwa ajili ya manufaa ya vizazi vijavyo ni vyema wenyeviti wa vijiji na watendaji wa kata kuwa wawazi pindi inapoletwa miradi ya maji ili mwananchi atunze kitu anachokiona kuliko kufichwa.
Amesema viongozi hao wanatakiwa kutoa hamasa kubwa juu ya kulinda miradi hiyo na kuongeza kuwa serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi kwa ajili ya huduma ya maji hivyo viongozi wanatakiwa kuwajibika ipasavyo ili kuhimiza utunzaji wa vyanzo vya maji.
Godfrey Methsela ni mwezeshaji FAHODE amesema endapo miradi hiyo ikiwekwa wazi itasaidia wananchi kuelewa miradi hiyo inavyoenda bila ya kubaki na maswali mengi na kuongeza kuwa mabadiliko mengi yameonekana tangu kuanzishwa kwa shirika hilo kupitia mikutano ya adhara pamoja na midahalo.
Kwa upande wake Jovin Rutainurwa mgeni rasmi katika mdahalo huo aliyemwakilisha mkuu wa wilaya ya Bukoba amezitaka kamati za maji kutengeneza timu za watu waaminifu kuliko wale aliowaita wapiga dili wanatumia vibaya nafasi zao kujinufaisha wao wenyewe baada ya miradi ya maji kufika katika maeneo yao kuacha tabia hiyo Mara moja tabia hiyo kwani kwa kufanya hivyo ni kosa kisheria.
Shirika hilo linatoa huduma katika sekta za maji katika kata za halmashauri ya wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera ikiwa no pamoja na Katoma, Katoro,Kemondo, Maruku, Ibwera na Katerero.
Hata hivyo akizungumzia shirika hilo Bwana Justo Mutabuzi ambaye ni afisa wakala wa maji vijijini Ruwasa ametoa pongezi kwa shirika hilo kwa jitihada zake kwa jamii na kuwahimiza watendaji kutokuwa waoga kwa baadhi ya watu wanaohujumu na kuharibu miradi ya vyanzo vya maji.
No comments:
Post a Comment