HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 19, 2020

TAMASHA LA KUOMBEA UCHAGUZI MKUU 2020 KURINDIMA JUMAPILI HII UWANJA WA UHURU

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Agosti 19, 2020 wakati wa kutambulisha Tamasha la kuombea Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, litakalofanyika Agosti 23, 2020 kwenye Uwanja wa Uhuru.
Baadhi ya waandishi wa habari wakichukua matukio wakati wa kutambulisha Tamasha la kuombea Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, litakalofanyika Agosti 23, 2020 kwenye Uwanja wa Uhuru.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Agosti 19, 2020 wakati wa kutambulisha Tamasha la kuombea Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, litakalofanyika Agosti 23, 2020 kwenye Uwanja wa Uhuru.

 

DAR ES SALAAM, TANZANIA

KAMPUNI ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam, imeandaa Tamasha la Maombezi lisilo la kiingilio la kuombea Uchaguzi Mkuu wa Tanzania utakaofanyika Oktoba 28, 2020, linalotarajiwa kupambwa na waimbaji mbalimbali, akiwemo Rose Mhando.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Alex Msama, alisema lengo la tamasha hilo, litakalofanyika Jumapili hii ya Agosti 23 kwenye Uwanja wa Uhuru, Temeke, Dar, ni kumkabidhi Mungu mchakato huo muhimu kwa taifa.

“Msama Promotions tumeona tuandae tamasha la Kuombea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, mwaka huu, ili ufanyike kwa amani na utulivu. Watakuwepo waimbaji, maaskofu, wachungaji, viongozi wa Serikali na wa madhehebu mbalimbali.

“Kama tulivyopitia magumu menngine na Mungu akatuvusha salama, tunaamini tunapaswa kujielekeza kwake ili atuvushe pia katika hili la Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani,” alisemna Msama na kuwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi.

Akidokeza waimbaji watakaotumbuiza katika tamasha hilo lisilo na kiingilio, Msama aliwataja baadhi kuwa ni Bonny Mwaitege, Christopher Mwingira, Christina Shusho na Rose Mhando, ambaye atajibu maswali juu ya ukimya wake na kwaya mbalimbali.

“Nataka kuwaambia Watanzania kuwa, Rose Mhando yupo na Jumapili hii atakuwepo jukwaani pale Uwanja wa Uhuru. Ni muda mrefu hajaonekana, nawahakikishia yupo na yuko katika afya njema akiendelea na huduma ya uimbaji.

“Watanzania wajitokeze kwa wingi siku hiyo ili wapate sio tu kumuona akiimba, bali pia kusalimiana nae. Baada ya maswali mengi kuulizia aliko, Rose Mhando atakuja kuibukia katika tamasha hili la kuombea uchaguzi,” alibainisha Msama.

Alisisitiza kwamba, hakutakuwa na kiingilio, na kuwa tamasha hilo ni la bure, huku akisema ni juu ya kila mmoja kujitoa aliko yeye na familia yake, kwenda uwanjani kuungana na Watanzania wengine kushiriki tamasha hilo.

Msama Promotions imekuwa ikiratibu na kuendesha matamasha mengi makubwa nchini yanayoshirikisha waimbaji hata wa kimataifa, yakiwemo ya Pasaka, Krismasi na mengineyo, yanayoendana na matutino makuu yanayotokea.

No comments:

Post a Comment

Pages