HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 08, 2020

NMB Nane Nane Simiyu

 Katika maadhimisho ya Nane Nane kitaifa yaliyofanyika viwanja vya Nyakabindi Mkoa wa Simiyu, Benki ya NMB imewahakikishia wakulima kuwa wako nao pamoja ili kuhakikisha wanasonga mbele zaidi. Hata hivyo benki hiyo imepata fursa kubadilishana uzoefu na wakulima- namna nzuri ya kukuza kilimo chao na pia kuweza kuona fursa zilizopo.


Akielezea ni namna gani Benki hiyo inaunga mkono juhudi za serikali, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara - Filbet Mponzi alisema “Mchango wetu kama benki wakujenga Uchumi imara kupitia kilimo na ufugaji ni kuwa kwa mwaka huu, tumetoa zaidi ya TZS Bilioni 230 kama mikopo kwenye mazao ya Pamba, Korosho Kahawa, Katani, Tumbaku, Mihogo, Mchele na Mahindi”.


Pia, Kwa mwaka huu, NMB Imetenga TZS 1.9 billioni kwaajili ya ujenzi wa maghala (warehouse) kuhifadhi mazao ya
wakulima. Aidha, kupitia ‘NMB Foundation’ NMB imeweza kutoa elimu ya fedha na mafunzo ya biashara kwa vyama vya ushirika wa wakulima (AMCOS) 1550 nchi nzima, ili kuwajengea uwezo wa namna bora ya kusimamia mapato yao. 

Kwa Kanda ya Mashariki ya Ziwa (Shinyanga, Mara na Simiyu) wameweza kufikia AMCOs zaidi ya 700. Tangu 2016, NMB imetoa zaidi ya TZS 800 bilioni kusaidia kilimo na mnyororo wa thamani wa mazao ya kilimo.

No comments:

Post a Comment

Pages