HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 08, 2020

RAS Simiyu awataka Wanawake kuchangamkia fursa zinazotolewa na Benki ya CRDB ili waweze kujikomboa kiuchumi

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu Bi. Miriam Mmbaga awataka wanawake waungane na washirikiane na mabenki hasa Benki ya CRDB kwakuwa ni Benki ambayo imeonyesha nia ya dhati katika kumkomboa Mwanamke. 

 

“Wanawake wenzangu msipoungana mkaunda vikundi hamtaweza kufanikisha Malengo yenu, mkiwa katika vikundi ni rahisi kukopesheka na kuaminiwa na mabenki nchini” Bi. Mmbaga alisema hayo wakati akifungua mafunzo maalumu ya wanawake wajasiliamali yaliyoandaliwa na Benki ya CRDB na kuendeshwa na Bi Rachel Senni-Meneja Mahusiano Mwandamizi Kitengo cha Uwezeshaji wa Wanawake wa Benki ya CRDB yaliyofanyika wilayani Bariadi.

 Bi. Rachel Senni Meneja Mahusiano Mwandamizi Kitengo cha Uwezeshaji wa Wanawake-Benki ya CRDB akitoa mada kuhusu fursa za uwezeshaji kwa wajasiliamali wanawake Wilayani Bariadi-Simiyu.

Huu ni mwendelezo wa mpango mkakati ambao Benki ya CRDB inaufanya katika kuhakikisha inawafikia wanawake wengi nchini ili kuwainua kiuchumi na kuongeza chachu ya maedeleo ya kijamii na Taifa kwa ujumla.
 
 Aidha Bi. Mmbaga aliishukuru Benki ya CRDB kwa kuwa mdau mkubwa kuinua maendeleo ya Mkoa wa Simiyu na Taifa kwani aliitaja CRDB Benki kuwa ni Benki ya kwanza ya kizalendo Nchini inayotoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya Taifa kwa kuwawezesha makundi mbalimbali hasa ya akina Mama nahivyo kuwa chachu ya maendeleo ya Tanzania kuufikia uchumi wa kati.
 

 Benki ya CRDB imekuwa mstari wa mbele katika kushiriki kumkwamua mwanamke kwa kuhakikisha inatoa fursa zinazoleta mafanikio kwa wanawake wa kada zote. 

 

Benki ya CRDB inafanya hivyo kwa kubuni bidhaa na huduma maalum za kifedha kwa ajili ya wanawake ikiwamo huduma za akiba na mikopo, Programu za mafunzo kwa wanawake (SME Tool Kit).Naye Bi Tano Mwera Mkuu wa Wilaya ya Busega aliwataka wanawake wa mkoa wa Simiyu wasikubali kuachwa nyuma, badala yake wajikite katika kuchangamkia fursa mbalimbali zitolewazo na Benki ya CRDB ili waweze kukuza uchumi wao lakini pia kulisaidia taifa katika kusukuma gurudumu la maendeleo.


“CRDB Benki inatambua ushiriki wa wanawake na hili ni moja ya vichocheo muhimu katika ukuaji na mafanikio ya kiuchumi ya jamii na nchi kwa ujumla naomba akina mama changamkieni fursa hizi.” Aliongeza Bi. Tano Mwela.
 

Benki ya CRDB mapema mwaka huu ilizindua rasmi akaunti ya wanawake ijulikanayo kama Malkia akaunti na kuja na suluhisho la kilio cha muda mrefu cha wanawake kuhusiana na riba, ambapo Benki imepunguza riba inayotoza katika mikopo ya wanawake wajasiriamali kutoka asilimia 24 hadi kufikia asilimia 14. 

 

Hili ni punguzo kubwa sana ambalo limedhamiria kutoa unafuu wa mikopo na kuongeza wigo wa kukopa kwa wanawake Nchini. Katika Mafunzo hayo akaunti zaidi ya 100 zilifunguliwa na akina mama hao.

No comments:

Post a Comment

Pages