HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 08, 2020

DC JOKATE AWAFUNDA VIJANA WANAOSHIRIKI KATIKA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA KISARAWE

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo, kulia akizungumza jambo na baadhi ya  maofisa wa Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) mara baada ya kumalizika kwa halfa fupi ya ufunguzi wa mafunzo ya jeshi la akiba (Mgambo) kwa vijana wapatao 150 kutoka Wilaya hiyo nyuma ni mwonekano wa baadhi ya washiriki katika mafunzo hayo.(Picha na Victor Masangu).
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo (kulia) akiwa wameketi meza kuu sambamba na viongozi wengine mbali mbali wa serikali pamoja na maofisa wa JWTZ wakati wa ufunguzi wa sherehe za mafunzo ya jeshi la akiba kwa vijana wa kisarawe kushoto kwake ni Mshauri wa jeshi la akiba Wilaya ya Kisarawe Meja Mohamed Wawa.(Picha na Victor Masangu).

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe akiwa katika picha ya kumbukumbu na viongozi mbalimbali pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo.

 

VICTOR MASANGU, KISARAWE

VIJANA ambao wanamaliza  mafunzo mbali mbali ya jeshi la akiba  wametakiwa  kuwa wazalendo na nchi yao kwa kuhakikisha wanalinda na kutunza rasilimali zote za Taifa na kuachana kabisa  kushiriki katika makundi ya vijiweni na  badala yake wajikite zaidi katika  kulinda hali ya amani na utulivu kwa wananchi pamoja na kushiriki katika shughuli za kimaendeleo .

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mafunzo  hayo ya jeshi la akiba amabyo yamehudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali amewataka pia kulivalia njuga suala la changamoto ya wanafunzi kupata mimba za utotoni na kupelekea kukatisha masomo yao pamoja na kutofumbia macho vitendo vya  ubakaji kwa watoto.

“Mimi kama Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe napenda kuwaasa vijana wote ambao mmepata fursa ya kushiruki katika mafunzo haya ya jeshi la akiba kwa muda wa miezi minne, kikubwa nataka pindi mtakapokamilisha kozi hii ni lazima kwama muwe wazalendo na nchi yenu na kuhakikisha kwamba mnasimamia na kutunza rasilimali zote za Taifa la Tanzania,”alisema Joketi.

Aidha alisema kwamba ana imani kubwa na vijana hao wataweza kuzingatia mafunzo mbali mbali ambayo watayapata katika kipindi chote hicho na kuwakumbusha mambo muhimu ambayo wanayotakiwa kufayafanya  ikiwemo kulinda hali  amani na utulivu hasa katika kipindi chote cha  kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2020.

“Napenda kuwakumbusha kwa sasa ni kipindi cha uchaguzi mkuu wa ngazi mbali mbali ikiwemo udiwani, nafasi za ubunge na Urais kwa hivyo ninawaomba sana kuweni makini katika kipindi hiki kwani mnaweza kurubuniwa na watu mbali mbali kwa hivyo ninawaoba sana kuweni makini ili wilaya yetu ya Kisarawe iwe salama na uchaguzi umalizike bila ya kuwa na tatizo lolote,”alisisitiza.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Wilaya alibainisha kwamba vijana wote ambao wanashiriki katika mafunzo hayo ya jesho la akiba ni lazima wahakikishe wanakuwa na kadi za kupigia kura kwani ni haki yao ya msingi ya kumchagua kiongozi yoyote kwa lengo la kushirikiana naye katika kuleta chachu ya maendeleo katika Nyanja mbali mbali.

Awali akisoma risala katika ufunguzi huo Mshauri wa jeshi la akiba katika Wilaya ya Kisarawe Meja Mohamed  Wawa alibainisha kwamba  vijana ambao wanashiriki katika mafunzo hayo wapo 150 na kwamba  watafundishwa  mambo mb ali mbali ikiwemo kulinda hali ya amani na ulinzi wa nchi yao huku akidai baadhi yao wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa yeti vya kuzaliwa.

 Nao baadhi ya  vijana ambao washiriki mafunzo hayo akiwemo Helihuruma Lifa na Eliwaza Saimon walisema kwamba  mafunzo hayo watayatumia vema na  uweledi mkubwa katika kuhakikisha wanatekeleza maagizo yote waliyopatiwa na Mkuu wa Wikaya ikiwemo kulinda rasirimali za taifa pamoja na kudumisha hali ya ulinzi na usalama kwa wananchi kwa kuzingati hseria na taratibu za nchi.

Mafunzo hayo  ya jeshi la akiba kwa vijana  wapatao 150 wasichana na wavulana kutoka Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani yatachukua kipindi cha miezi minne ambapo yanatarajiwa kumalizika  rasmi Novemba  2 mwaka huu.

                                        

No comments:

Post a Comment

Pages