HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 04, 2020

TANESCO YAMUHAKIKISHIA WAZIRI KAIRUKI UMEME WA KUTOSHA NA WA UHAKIKA KWA WAWEKEZAJI

Na Mwandishi Wetu, Simiyu

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO)  limemuhakikishia Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji, Mhe. Angellah Kairuki kuwa umeme upo wa kutosha na wa uhakika kwa wawekezaji.

Waziri Kairuki alipewa hakikisho hilo na Meneja wa TANESCO Mkoa wa Simiyu, Mhandisi Khadija Abdullahmed, wakati kiongozi huyo alipotembelea banda la shirika hilo kwenye maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Nyakabindi nje kidogo ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.

Hakikisho hilo lilikuja baada ya Mhe. Kairuki kuuliza TANESCO mnao umeme wa kuwatosheleza wawekezaji?, na ndipo Mhandisi, Khadija akamuondoa hofu kwa kusema “Mheshimiwa Waziri TANESCO tunao umeme wa kutosha na wa uhakika kukidhi mahitaji ya uwekezaji na wawekezaji.”

Kauli mbiu ya mwaka huu ya maonesho hayo yanayofanyika mkoani Simiyu kwa mwaka wa tatu mfululizo ni “Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Chagua Viongozi Bora 2020.”
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji, Mhe. Angellah Kairuki (kulia) akipatiwa maelezo na Meneja wa TANESCO mkoa wa Simiyu, Mhandisi Khadija Abdullahmed alipotembelea banda la TANESCO kwenye maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Nyakabindi nje kidogo ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu leo Agosti 3, 2020.

No comments:

Post a Comment

Pages