HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 05, 2020

TECNO YAZINDUA PROMOSHENI YA 'VIMBA SEASON'

* WASANII WA TAMTHILIYA YA HUBA WAWA GUMZO
Meneja mauzo wa kampuni ya simu ya TECNO akiwa ameshika TECNO CAMON 15 na Spark 5 alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Wasanii wa tamthilia ya Huba waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Promosheni ya TECNO Vimba Season jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja ikimwonesha pia msanii wa vichekesho maarufu Pierre Liquid mbele (katikati).


Na Janeth Jovin

Kampuni ya simu za mkononi ya TECNO imezindua promosheni maalum ijulikanayo kwa jina la 'TECNO Vimba Season'  huku hafla hiyo ikihudhuriwa na wasanii maarufu wa tamthiliya ya HUBA ambayo huoneshwa na king’amuzi cha Dstv.

Promosheni hiyo ya ‘Vimba Season’ iliyozinduliwa jana inalenga kuwapatia wateja wake wa simu ya  TECNO CAMON15 na Spark5 zawadi mbalimbali ikiwemo seti ya king’amuzi cha Dstv kilicholipiwa chaneli za kifurushi cha familia kwa mwezi mzima.

Pia wateja wa simu hizo watapata nafasi ya kuingia moja kwa moja kwenye droo ya  shindano la zawadi kubwa ya gari.

Akizungumza jana wakati wa hafla ya uzinduzi huo, Meneja Mauzo wa TECNO  Mariam Mohamed amesema promosheni hiyo ni mwendelezo wa promosheni ya Vimba Season ambayo hufanyika mara moja kila mwaka.

“Leo kwa mara nyingine tena tumewaletea msimu wa promosheni ya Vimba Season na kwa mwaka huu simu ambazo zitaambatana na zawadi ni TECNO CAMON 15 na Spark5. Kwahiyo mteja yeyote atakayenunua CAMON15 au Spark 5 ana uwezo wa kuingia moja kwa moja kwenye droo yetu kubwa ya kushinda gari” amesema Mariam.

Mariam aliongeza kuwa, “Pia tumeshirikiana na Dstv kwa mara nyingine tena, kwahiyo ukinunua simu hizi CAMON15 au Spark5 unapata Dstv na promosheni yetu inaanza rasmi leo nchi nzima.”   

Kwa upande wake Meneja Masoko wa TECNO, William Motta amesema kuwa promosheni hiyo itafanyika kwa muda wa mwezi mzima nchini kote katika maduka ya TECNO hivyo amewaomba   wateja wa TECNO na watanzania kwa ujumla kutoikosa kwani ni fursa kwa kila mmoja.

No comments:

Post a Comment

Pages