NA ABDALLAH HIJA
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limezitaka klabu kumaliza usajili
mapema huku wakisistiza hawatoongeza muda kwenye dirisha hilo endapo
likifungwa.
Dirisha hilo la usajili linahusisha klabu zote za Ligi Kuu Tanzania Bara
(VPL), Daraja la kwanza (FDL), la Pili (SDL) na ile ligi kuu ya
wanawake wakati linaelekea tamati likiwa limebakisha siku tano kufungwa
kwa pazia lake.
Akizungumzia hilo Ofisa Habari wa TFF, Cliford Ndimbo alisema, zimebakia
siku chache kufungwa kwa dirisha la usajili kikubwa bado wanaendelea
kusistiza klabu kufanya jambo hilo kwa wakati, kwa sababu hakutakuwa na
muda wa ziada endapo zoezi litafungwa.
“Tayari tushafanya ‘setting’ kwa mameneja wa mitandao hiyo ya Transfer
Matching System (TMS) kuwakumbusha suala zima la usajili na uhammisho
hakuna changamoto yoyote iliyokumba klabu, lakini tumetoa nafasi kama
kuna changamoto yoyote kuwasiliana na idara ya mashindano ya TFF ili
kuweza kupata msaada,” alisema Ndimbo.
No comments:
Post a Comment