NA ABDALLAH HIJA
UONGOZI wa Mabingwa wa Kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) Yanga
SC , umefunguka kuwa unaangalia namna ya kusogeza muda kwenye michezo
yao itakayopamba kilele cha wiki ya Wananchi ili kuupa heshima mtanange
wa ngao ya jamii.
Mchezo huo wa ngao ya jamii utakaopigwa saa 9 alasiri, Agosti 30 mwaka
huu, utakaowakutanisha Simba SC dhidi ya Namungo Uwanja wa Sheikh Amri
Abeid jijini Arusha, utaambatana na shughuli ya kilele cha wiki ya
Wananchi itakayofanyika Dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga Hassani Bumbuli michezo katika wiki
ya wanachi itachezwa mara baada ya kumalizika ule wa ngao ya jamii huku
mechi iliyokuwa ikisubiliwa kwa hamu Kati ya Yanga dhidi ya Aigle Noir
ya Burundi itapigwa saa 1 jioni.
Bumbuli alisema, kwa kuheshimu ufunguzi wa ligi kwa mchezo wa ngao ya
jamii wanajaribu kusogeza ratiba yao kwa muda ule wa saa tisa na hadi
dakika 90 zinakamilika kusiwepo na mechi yeyote.
“Tunajaribu kutoa heshima kwa mchezo wa ufunguzi ili
kuheshimu pazia la ligi linafunguliwa, tutajaribu kuangalia uwezekanao
wa kufanya hivyo vitu vingine tutajaribu kuangalia hapo baadae,” alisema
Bumbuli.
No comments:
Post a Comment