HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 31, 2020

Wana CCM Michungwani waaswa kutochagua wapinzani

Na Asha Mwakyonde

 
MGOMBEA mteule wa udiwani Kata ya Saranga Wilaya ya Ubungo Edward Laiser amewataka Wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Tawi la Michungwani kufanya maamuzi sahihi ya upigaji kura za ndio kwa wagombea wa chama hicho.
 

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana katika mkutano mkuu wa tawi hilo Laiser alisema lakini  hana wasiwasi na wnana CCM wa tawi hilo kwani ni moja ya matawi ambayo hayajawahi kumuangusha Rais John Mgufuli katika kumpigia kura za ndio.


Laiser alisema Wanamichungwani wakichagua mafiga matatu kwa maana diwani, Mbunge na Rais wa CCM maendeleo yatapatikana  kwani tangu ilivyopokelewa Wilaya ya Ubungo kutoka Kinondoni hakuna maendeleo yoyote yaliyofanyika kutokana na upinzani uliokuwapo.


Alisema hakutakuwa na maendeleo yoyote  katika kata ya Saranga kama wanachama wa CCM watakosea kuwachagua wapinzani kama walivyofanya katika uchanguzi wa 2015.
Laiser aliongeza  kuwa kilichosababisha diwani aliyemaliza muda wake Yusuph Mdoe ashindwe kutatua changamoto za kata hiyo ni wananchi walikosea katika upigaji kura kwani hawakuweza kufanya maamuzi sahihi.


alisema Mdoe hakuweza kuongea lugha moja na wapinzani  ambao ndio walioshika Halmashauri ya Ubungo kwani fedha zote walizishikilia wapinzania hao.


"Mambo mengi hayataweza kufanyika kama kutakuwa na viongozi mchanganyika katika jimbo la Ubungo hivyo wanaccm chagueni mafiga matatu yaani Rais, Makamu wa Rais na diwani wote wa CCM,"alisema Laiser.


Alisema Jimbo la Ubungo  na kata ya Saranga kwa ujumla hakuna maendeleo kutokana na upinzani uliokuwa umetawala kipindi cha miaka kumi.


 "Tumpe Rais Magufuli  kura za ndio nyingi ili aweze kutufanyia
maendeleo makubwa mpeni mbunge na diwani wa CCM ili aweze kutuletea maendeleo kwani yaliyokuwepo amefanya kwa huruma tu," alisema.


Alisema  wanaccma wakikosea kupiga kura na kuwapatia upinzania hakuna maendeleo yoyote yatakafanyika katika kata ya Saranga na jimbo la Ubungo.


"Mchanganuo wa miradi ya serikali ni mkubwa katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo hayataweza kufanyika endapo wanamichugwani mkileta kirusi cha upinzani katika mfumo wa uongozi,"alisema Laiser.
 

Laiser alisema akina mama na vijana hawapati fedha za mikopo kutokana na upinzani hawakuweza kuzungumza lunga moja na diwani wa CCM aliyemaliza muda wake Yusuph Mdoe.
Wazee Alisema kuwa wazee ndiyo hazina yao na kwamba wapo tayari kukaa  nao ili waweze kushauriwa mambo muhimu katika kuelekea uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika Oktoba 28, mwaka huu.


"kwanza tunachukua fursa hii kuwaomba radhi wazee wetu  ambao ndio hazina yetu, chaguzi zote zilizopita hatujatambua nafasi za wazee na ndio maana hakutuweza kufanya vizuri uchaguzi uliopita katika jimbo letu," alisema.


Alisema kuwa uchaguzi huu wanahitaji kuishirikisha kamati ya wazee ili kupata busara zao kuelekea uchaguzi mkuu na kuweza kuwashauri mambo muhimu yatakayosababisha ushindi.
Aliongeza kuwa wazee hao wamekaa ndani ya CCM miaka na kuitumikia serikali kwa miaka mingi  hivyo wanafahamu mengi wanaweza kuwaelekeza mambo ya msingi ili waweze kushika dola.


Alisema chama cha siasa chochote kile kinatafuta dhamana ya kushika dola hivyo kama CCM hawawezi kukubali  chama hicho kikashindwa kushika dola kwa uzembe wa watu wachache.

No comments:

Post a Comment

Pages