Makamu Mwenyekiti Jumuiya ya wanawake wa Chama cha Wananchi CUF ambaye pia ni mbunge viti maalumu aliyemaliza muda wake Mkoa wa Kigoma Kiza Mayeye kushoto akizungumza na wanahabari
Na Asha Mwakyonde
WANAWAKE wa Jumuiya ya Chama cha Wananchi (CUF), wamechangia kiasi cha Sh. Milioni 1, Mwenyekiti wa chama hicho Prof. Ibrahimu Lipumba kwa ajili ya kuchukulia fomu ya kugombea nafasi ya urais Oktoba mwaka huu.
Haya yamesemwa jijini Dar es Salaam jana na Makamu Mwenyekiti Jumuiya ya wanawake wa Chama hicho ambaye pia ni mbunge viti maalumu aliyemaliza muda wake Mkoa wa Kigoma Kiza Mayeye amesema wanaamini Prof. Lipumba anafaa.
Kiza amesema baada ya Mwenyekiti huyo Prof. Lipumba kuamua kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya urais Oktoba mwaka huu wao kama wanawake waliona ni vema wakachanga kwani wanaamini ndiye rais anayefaa kushika dola.
Amesema kuwa wao kama wanawake wa jumuiya ya chama hicho wanaamini Prof. Lipumba ndiye tumaini lao ndiyo maana wamemua kuchanga fedha kwa ajili ya kuchukulia fomu.
Amesema kuwa wanawake wa chama hicho kwa kushirikiana wamechanga na kupata kiasi cha Sh. Milioni 1 na kumkabidhi Prof. Lipumba ili aende jijini Dodoma kuchukua fomu hiyo. 'Sisi kama wanawake wa chama cha wananchi Cuf tutakuwa pamoja naye kumpeleka jijini Dodoma kuchukua fomu ya urais Agasti 10 mwaka huu,' amesema Kiza.
Ameongeza kuwa kampeni zitakapoanza watakuwa na gombea wao wa kiti cha urais na kwamba watahakikisha wanatafuta kura mchana na usiku ili kuhakikisha chama hicho kinashika dola.
No comments:
Post a Comment