HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 14, 2020

AJALI YA MOTO YAUA WANAFUNZI 10

 Na Lydia Lugakila Kagera

Jumla ya wanafunzi 10 wamefariki dunia katika ajali ya moto iliyotokea  katika Shule ya Msingi Islamic (Byamungu) iliyopo kata ya Itera wilayani Kyerwa mkoani Kagera.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ambaye ni Mkuu wa wilaya hiyo, Rashid Mwaimu, amesema kuwa Moto huo umetokea usiku wa kuamkia leo.

Amesema kuwa chanzo cha moto huo hakijajulika na tayari vyombo vya ulinzi na usalama vimefika katika eneo la tukio.

Mabaki ya shule ya  Shule ya Msingi Islamic (Byamungu).

No comments:

Post a Comment

Pages