HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 15, 2020

MGAWE - CHADEMA TUNAENDA KUMALIZA CHANGAMOTO YA UPATIKANAJI WA MAJI JIMBO LA KIBAMBA


Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika (kulia) akimnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Kibaha, Ernest Mgawe, akimwombea kura kwa wananchi  wakati wa ufunguzi wa kampeni zilizofanyika katika viwanja kimara stop over.


Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kibamba kupitia CHADEMA, Ernest Mgawe, akizungumza jambo na kuwaomba  wananchi ridhaa ya kumchagua wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni hizo ambazo zilihudhuliwa na viongozi mbali mbali kutoka ngazi za chini hadi ngazi ya Taifa kwa ajili ya kuomba kura.

 

 

NA VICTOR MASANGU, MBEZI 

 

Mgombea wa  ubunge katika jimbo la Kibamba Ernest Mgawe kupitia tiketi ya Chadema  amesema kwamba  endapo atapata nafasi ya kuchaguliwa na wananchi  katika uchaguzi  wa mwaka huuu atahakikisha kwamba analivalia njuga changamoto ya  upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama ili kuwaondolea   wananchi kero na adha kubwa ya kutembea umbari mrefu kwenda kutafuta maji hususan kwa wakinamama.

Mgawe aliyasema hayo wakati wa uzinduzi rasmi wa kuanza kwa kampeni yake iliyofanyika katika viwanja vya kimara stop over kwa ajili ya   kuwaomba ridhaa wananchi kumpatia nafasi hiyo ili kuwawakilisha bungeni kwa ajili ya kupeleka kero  na  changamoto mbali mbai  ambazo zinawakabili lengo ikiwa kuzitafutia ufumbuzi.

Aidha Mgombea huyo alisema kwamba lengo lake kubwa ni kushirikiana na viongozi wake  kwa lengo la kuweza kuhakikisha kwamba wanatatua changamoto na kero mbali mbali ambazo zinawakabili wananchi wake ikiwemo kusimamia miradi ya maendeleo katika sekta ya maji, miundombinu ya barabara pamoja na mambo ya afya.

“Katibu wangu wa Chama Mnyika ameongelea mambo mbali mbali lakini nipende kuwaambia wananchi kitu kikubwa ambacho kinatakiwa ni kunichagua mimi ili niwe Mbunge wa Jimbo la Kibamba na zile changamoto mbali mbali za mambo yanayohusina na sekta ya ardhi upatikanaji wa maji safi na salama ikiwemo suala la asilimia 10 ambazo zinatolewa katika makundi ya vijana, wakinamama na walemavu zinatolewa kwa usawa ili ziweze kuwanufaisha wate,”alisema Magawe.

Katibu Mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo Taifa  (CHADEMA) John Mnyika amewataka wagombea wa nafasi za udiwani na ubunge  endapo wakishinda katika uchaguazi mkuu wa mwaka huu kuhakikisha wanasikiliza kero na changamoto mbali mbali ambazo zinawakabilia wananchi katika sekta mbali mbali ikiwemo suala la urasimishaji wa ardhi ili wananchi wapate hati zao miliki.

“Sasa hivi ndugu zangu tupo kwenye kampeni na tunaelekea kipindi cha uchaguzi kwa hiyo mimi nilipokuwa Mbunge wa Jimbo la Kibamba nililete mabadiliko makubwa ingawa kuna baadhi ya vitu vingine ilikuwa bado sijavimalizia ikiwemo ule mpango wa urasimishaji wa ardhi kwa wananchi na kupata hati zao hivyo ninamuomba sana Mgawe atachagulia jambo hili alifanyia kazi haraka,”alisema Mnyika.

Naye mmoja wa watoto wa Mgombea ubunge huyo Preshezeli Mgawe  hakusita kuonyesha hisia alizonazo mara baada ya kupanda  jukwaani na kumwombea kura baba yake mzazi na kuwaomba wananchi kumuamini kwani alipokuwa diwani wa kata ya kibamba aliweza kuleta chachu ya maendeleo kwa wananchi wake.

 

“Nimepanda katika jukwaa hili mimi napennda kumwombea baba yangu mpendwa haweze kuchaguliwa katika nafasi ya Ubunge jimbo la Kibamba ili aweze kushirikiana na viongozi na wananchi ili kuweza kuleta maendeleo nina waombeni sana kumpatia baba yangu kura nyingi ili aweze kuwaletea mabadiliko zaidi,”alisema Mtoto huyo.

Kwa upande wake Meneja wa mgombea huyo  Hunfrey Sambo aliwataka wanachama wa Chadema kuhakikisha wanazingatia sheria na taratibu zote  wakati wa kipindi cha kampeni pamoja na kuelekea katika uchaguai mkuu na kuwahimiza kwamba wawachagua viongozi wa nafasi zote tatu kuaniza udiwani, Ubunge na nafasi ya Urais kupita tiketi ya Chadema.

No comments:

Post a Comment

Pages