HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 13, 2020

MGOMBEA MWENZA WA CHADEMA AFIKA NYUMBANI KWA MAREHEMU DK. PHILEMON NDESAMBULO KUHANI KABURI LAKE

 

 Mjane wa aliyekuwa mwasisi wa CHADEMA, marehemu Dk. Philemon Ndesamburo, akimpa zawadi mgombea nafasi ya Makamu wa Rais kupitia Chadema, Salum Mwalimu, alipokwenda kuhani kaburi la marehemu Dk. Ndesamburo leo Septemba 13, 2020 mjini Moshi. 

 

Ndehorio Moshi ambaye ni mjane wa mwasisi wa CHADEMA, marehemu Dk. Philemon Ndesamburo, akimvisha skafu ya chama hicho mgombea mwenza kupitia CHADEMA, Salum Mwalimu, kama ishara ya kumtia nguvu alipofika nyumbani kwake Moshi, Kilimanjaro kuhani kaburi la marehemu Dk. Ndesamburo.  


Mjane wa aliyekuwa  mwasisi wa Chadema marehemu Dk. Philemon Ndesamburo akimuongoza mgombea mwenza kupitia CHADEMA, Salum Mwalimu, kwenda kuhani kaburi la marehemu Dk. Ndesamburo.  

Mgombea mwenza kupitia CHADEMA, Salum Mwalimu (katikati), akiongoza dua ya kumuombea mwasisi wa chama hicho marehemu Dk. Philemon Ndesamburo, nyumbani kwake Moshi Kilimanjaro, Septemba 13, 2020.  Kushoto kwake ni mjane wa marehemu, Ndehorio Moshi.
Mgombea mwenza kupitia CHADEMA, Salum Mwalimu, akiagana na mjane wa aliyekuwa mwasisi wa CHADEMA, marehemu Dk. Philemoni Ndesamburo, baada ya kuhani kaburi lake leo Septemba 13, 2020, Moshi Kilimanjaro.

No comments:

Post a Comment

Pages