Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akiwa ameketi mbele kwenye gari aina ya Lori ambalo limeunganishwa na kiwanda cha GFA kilichopo eneo la Tamko wilayani Kibaha wakati wa ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kukagua shughuli mbalimbali zinazofanywa na kiwanda hicho ikiwa ni kuunga juhudi za Rais Dk, John Pombe Magufuli.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo (katikati), akiwa ameongozana na baadhi ya viongozi wa kiwanda cha GFA kinachojishughulisha na uunganishaji wa magari aina ya malori wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua mwenendo wa uendeshaji kushoto kwake ni Meneja wa kiwanda hicho Ezra Mereng.Meneja wa cha GFA Ezra (kushoto) akiwapa anatoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evasist Ndikilo ambaye alifanya ziara yake ya kikazi katika kiwanda hicho kwa lengo la kujionea kazi mbali mbali pamoja na kusikiliza chanagmoto ambazo zinawakabili wawekezaji ili kuzitafutia ufumbuzi.(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU).
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
SERIKALI mkoani Pwani imewataka wawekezaji mbali mbali wa ujenzi wa viwanda kuhakikisha kwamba wanazingatia sheria na taratibu zote zilizowekwa ikiwemo kulinda maslahi ya wafanyakazi wao pamoja na kuwahudumia ipasavyo hasa pindi wanapokumbwa na majanga wakiwa katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku.
Kauli hiyo imetolew na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo wakati wa zira yake ya kikazi yeye lengo la kukagua na kutembelea baadhi ya viwanda vilivyojengwa katika Wilaya ya Kibaha ikiwemo kiwanda cha kuunganishia magari aina ya malori kinachojulikana kwa jina la GFA kilichopo eneo la Tamco Wilayani Kibaha pamoja na kusikiliza changamoto amabzo zinawakabili ili kuzifanyia kazi.
ametoa rai kwa wamiliki wa Viwanda ndani ya Mkoa huo kuzingatia haki na maslahi ya wafanyakazi wao.
Katika ziara hiyo Ndikilo alisema kwamba lengo la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha kwamba inaendelea kuwasaidia kwa hali na mali wawekezaji wote wazalendo na wal wengine wa nkje ili kuja kuwekeza kujenga viwanda mbali m ali ambavyo vitaweza kuleta mabadiliko makubwa ya kimaendeleo kwa wananachi wa Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani pamoja na Taifa kwa ujumla.
Aidha Mhandisi Ndukilio aliongeza kuwamba kukamilia kwa ujenzi wa kiwanda hicho kutaweza kutoa fursa mbali mb ali za ajira kwa vijana kutokana na kuweza kupata kazi m ali mbali ambazo zitaweza kuwasidia kujikwamua kuchumi na kuendesha maisha yao .
“Kikubwa mimi ammbachoi ninawaomba wamiliki wa viwanda hivi pamoja na kumuunga mkoni Rais wetu katika ujenzi wa viwanda lakini ni lazima kabisa tuhakikishe kwamba tuanazingatia sheria na taratibu za kaiz kwa wafanyakazi ambao wanafanya kazi hizi kwa kuwa wanatakiwa wapatiwe stahhiki zao zote bila uonevu na kuwahudumia ipaswavyo pindi wanapohumia waakiwa kazini,”alisema Ndikilo.
Pamoja na hayo alifafanua kuwa , katika ajira mbali mbali zinazotolewa kwa wafanyakazi zinatakiwa kuendana na haki ikiwemo vitendea kazi pamoja na maslahi na Afya zao wakiwa kazini.
" Baadhi ya wamiliki hawazingatii haki na maslahi ya wafanyakazi wao, wanawajali pale wanapokuwa wazima na kufanya kazi kwa bidii wakipata matatizo hawana habari nao, niwaombe kuheshimu wafanyakazi na kuwajali muda wote wakiwa kazini na wanazokumbana na matatizo" alisema Ndikilo
Aidha mkuu huyo wa mkoa aliwataka wamiliki hao wa Viwanda kutumia benki zilizopo ndani ya mkoa huo, kupitisha fedha zao na kuomba mikopo lengo kukuza pato la Mkoa huo na Taifa kwa ujumla.
Alitoa wito kwa Taasisi wezeshi za Mkoa huo kujipanga vizuri kutoa vibali kwa wawekezaji ili shughuli za Uwekezaji zifanyike kwa wakati.
Awali Meneja wa Kiwanda hicho, Ezra Mereng, alisema Kiwanda hicho Cha kuunganishiwa magari kitakapokamilika kitakuwa na Uwekezaji wa zaidi ya bilioni 12.
Katika hatua nyingine aliongeza kuwa malengo yao ya baadae ni kuwa na ajira 300 za moja kwa moja na zisizorasmi 700 ambapo kwa sasa zipo ajira 65 pekee na kwamba wataendelea kutoa ajira nyingine zaidi kulingana na mwenenndo wa uzalishaji ambavyo utakuwa ukiongezeka.
No comments:
Post a Comment