HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 01, 2020

Wataalamu wa Tiba asilia wampongeza Rais Magufuli, kumuombea Dua


Mivumo ya upepo inarindima kupeleka Tashtiti kwenye ukumbi wa Dkt. Ali Mohamed Shein ambapo wanafunzi wa UVCCM  vyuo na vyuo vya Elimu ya Juu Zanzibar wamekutana kwa ajili ya kufanya Mdahalo, kujadili kuhusu ushiriki wao kwenye Maendeleo ya Zanzibar.


NA JANETH JOVIN

 
WATAALAMU wa Tiba Asili kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania wamempongeza Rais Dk. John Magufuli kwa kuitambua na kuipa kipaumbele tiba hiyo hasa  katika mapambano ya ugonjwa wa Covid 19 hivyo kuahidi kumuombea Dua Oktoba 28 mwaka huu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Septemba Mosi, 2020, wakati wa mkutano maalum kwa ajili ya muendelezo wa maadhimisho ya siku ya tiba asili, Mwenyekiti wa Sauti ya Wataalam wa Tiba asili, Dk Juma Mwaka amesema tiba hiyo asili ni nyenzo iliyosaidia kupigana vita dhidi ya maradhi ya corona hapa nchini.

Amesema aliyetengeneza nyenzo hiyo ni Rais Magufuli hivyo kila mtanzania na mtaalamu wa tiba asili anapaswa kumshukuru rais kwani wakati mataifa mengine yakimbeza juu ya kauli yake hiyo yeye hakuona haya aliendelea na msimamo wake.

"Agosti 29, mwaka huu alipokuwa akizindua kampeni mjini Dodoma amesema tena atahakikisha kwamba wataalamu wa tiba asili tunambuliwa na si kubezwa hivyo nasi tuna kila sababu ya kumshukuru rais wetu na tunamuahidi hatutamuangusha," amesema Dk Mwaka.

Amesema wanafahamu na kuthamini namna ambavyo Rais Magufuli amejitoa kwa kuwaweka kwenye ramani ya kujulikana na kupewa heshima.

"Kutokana na hali inayoendelea hapa kwetu na duniani Kwa ujumla,  Shirika la Afya Duniani (WHO) limeanza kufuatilia takwimu za matumizi ya tiba za asili katika kutatua changamoto mbalimbali za afya" amesema Dk Mwaka na kuongeza

"WHO katika takwimu zao zimeonesha kuwa zaidi ya asilimia 80 ya watu kutoka katika mataifa  yanayoendelea wanatumia tiba asili na Kwa upande wa Tanzania tiba asili inatoa mchango wa zaidi ya asilimia 45 katika kutatua changamoto mbalimbali za afya," amesema na kuongeza

"Tunawaomba wataalamu wenzetu kutuunga mkono katika shukrani zetu na tumwombee katika safari yake Oktoba 25, mwaka huu," amesema Dk Mwaka.

Naye Mratibu wa Tiba asili kutoka Manisipaa ya Ilala, Dk Walter Macha aliiomba Serikali chini ya Rais Magufuli kutengeneza mazingira mazuri na wezeshi ili wazalishe bidhaa hizo Kwa wingi na kuziuza nje.

'Tunazo fursa nyingi za kiuchumi kwa kuwa tumezungukwa na nchi zinazotumia bidhaa za asili hivyo tunaomba tuwezeshwe ili kuongeza uzalishaji," amesema Dk. Macha.

Amesema wanafahamu Rais Magufuli kama ni mtu mwenye vipaji vingi ikiwa ni pamoja na uchapakazi, mwaminifu, mwadilifu, msomi, mwenye kumbukumbu, mkweli na mpenda maendeleo.

Aidha  Macha amesema Rais ana vipaji 11 alivyopewa na Mungu vikowemo mchapa kazi,mwaminifu,mwadilifu msomi kwenye kumbukumbu,mkweli na mpenda maendeleo.

"Naiomba serikali iboreshe mazingira ya uzalishaji Kwa bidhaa za asili Kwa kuwa mataifa yanayotuzunguka yanaamini katika matumizi ya bidhaa za asili,"amesema Macha

Kwa upande wake, mwakilishi kutoka Diaspora, Prince Katega amesema Mungu huleta watu wa aina ya Rais  kama Magufuli akikusudia kuleta mabadiliko muhimu Duniani.

"Tunamshukuru Rais kwa kusisitiza wataalamu wa tiba asili wasibezwe na wamesema anayeona tiba asili imepitwa na wakati ajue yeye ndio kapitwa na wakati hii ni kauli thabiti na ya kuungwa mkono," amesema Katega.

No comments:

Post a Comment

Pages