HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 15, 2020

NMB Ndani ya Dodoma

Benki ya NMB jana imeandaa hafla maalum jijini Dodoma ya kuwakaribisha Waheshimiwa Wabunge wote wa Bunge la 12, lililozinduliwa hivi karibu na Rais John Pombe Magufuli, kwa ajili ya kuwapongeza kwa kuchaguliwakuwawakilisha wananchi na kuwatakia safari njema katika kipindi cha miaka mitano ijayo. 

Naibu Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson akikaribishwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB Dk. Edwin Mhede.


Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna akimkaribisha Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania - Dk. Benard Kibesse. Wakishuhudia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki  ya NMB Dk. Edwin Mhede (kulia), Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB - Filbert Mponzi (kushoto) na Mkuu wa Idara wa Mawasiliano wa NMB - Eunice Chiume.
 
Hafla hiyo, ilizinduliwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. Tulia Ackson aliyekuwa Mgeni rasmi. Benki ya NMB ilitumia fursa hiyo kuwajulisha Waheshimiwa Wabunge namna wanaweza kufaidika na huduma nyingi za NMB ikwemo; mikopo maalum, uwekezaji, bima mbalimbali, na matumizi mbadala ya kibenki kama NMB Mkononi. 
Waheshimiwa Wabunge wakiburudika katika hafla hiyo.
Akizungumza kwa niaba ya Benki ya NMB, Afisa Mkuu Mtendaji, Bi. Ruth Zaipuna alisema, moja ya malengo ya Benki hiyo ni kuhakikisha wanashirikiana na wadau katika kujenga taifa bora lenye uchumi imara kupitia sekta ya kibenki. Dhamira ya NMB ni kuendelea kushiriki katika miradi ya maendeleo katika majimbo yao na taifa kwa ujumla. Vile vile, Dk. Tulia aliipoongeza Benki hiyo kwa kuendelea kuboresha huduma zake na kujitanua kiutendaji katika kila eneo hapa nchini huku akitambua mchango wa NMB katika jamii.
Wakiwa Dodoma, Zaipuna na Mponzi walishuhudia uzinduzi wa Bunge la 12, na vile vile kupata nafasi ya kumtembelea Kamishna Generali wa Magereza nchini – Suleimani Mzee katika ofisi yake.

No comments:

Post a Comment

Pages