HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 16, 2020

Timu ya wasichana U-17 yarejea nchi na ubingwa COSAFA

Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) Wales Karia akiwapokea wachezaji wa timu ya Taifa ya wasichana wa chini ya umri wa miaka 17 (U-17) mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Wachezaji hao wamerejea nchini wakiwa mabingwa wa michuano Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Kusini mwa Afrika, (COSAFA) baada ya kuwafunga Zambia kwenye fainali za mashindano hayo kwa mikwaju ya penati 3-4 kufuatia sare ya 1-1 mchezo uliofanyika uwanja wa Nelson Mandela Bay, Afrika Kusini.

Mabingwa wa michuano Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Kusini mwa Afrika (COSAFA) timu ya Taifa ya wasichana chini ya umri wa miaka 17 (U-17) wakishangilia
ushindi walioupata dhidi ya timu ya Zambia kwa kuwashinda kwa mikwaju ya penati 3-4 kufuatia sare ya 1-1 mchezo ulifanyika uwanja wa Nelson Mandela Bay, Afrika Kusini.
Mwenyekiti wa Soka la Wanawake nchini Bibi Amina Karuma akiwapokea wachezaji wa timu ya Taifa ya wasichana wa chini ya umri wa miaka 17 (U-17) mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam wakitokea Afrika Kusini waliposhiriki michuano Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Kusini mwa Afrika, (COSAFA) na kuibuka mabingwa.
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wales Karia (aliyebeba kombe) akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Taifa ya wasichana wa chini ya umri wa miaka 17 (U-17) mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam wakitokea Afrika Kusini waliposhiriki michuano Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Kusini mwa Afrika, (COSAFA) na kuibuka mabingwa.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Addo Komba (aliyebeba kombe) akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Taifa ya wasichana wa chini ya umri wa miaka 17 (U-17) mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam wakitokea Afrika Kusini waliposhiriki michuano Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Kusini mwa Afrika, (COSAFA) na kuibuka mabingwa.
Wachezaji wa timu ya Taifa ya wasichana wa chini ya umri wa miaka 17 (U-17) wakishangilia ushindi wao walioupata Afrika Kusini waliposhiriki michuano Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Kusini mwa Afrika, (COSAFA) mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam wakitokea na kuibuka mabingwa. (Na Eleuteri Mangi, WHUSM-Dar es Salaam).

No comments:

Post a Comment

Pages