HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 16, 2020

ZAWADI NBC MARATHON 2020

WAKATI joto la Mbio za Kimataifa za NBC Marathon zinazotarajiwa kufanyika Novemba 22 jijini Dodoma likizidi kupanda, zawadi kwa washindi zimewekwa hadharani.
 

NBC Dodoma Marathon inatarajiwa kujumuisha Mbio za Kilomita 42, Kilomita 21, Kilomita 10 na Kilomita 5 maarufu kama ‘Fun Run’.

 

Maandalizi yanakwenda vema na tayari wanariadha mbalimbali maarufu kutoka ndani na nje ya nchi wamekwishajisajili.

 

NBC Marathon ambayo inaendeshwa kwa ushirikiano kati ya Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), huku ikitarajiwa kushirikisha washiriki 3,000.

 

Mshindi wa kwanza katika Mbio za Kilomita 42 kwa upande wa wanaume na wanawake ataondoka na kitita cha Sh. 3,500,000 kila mmoja huku wa pili akijitwalia Sh. 2,500,000 wa tatu 1,500,000 wa nne Sh. 1,000,000 huku wa tano akijitwalia Sh. 750,000 wakati wa sita hadi kumi wakiondoka na Sh. 500,000 kila mmoja.

 

Kwa upande wa Kilomita 21 mshindi atajipatia Sh. 2,500,000 wa pili 1,500,000 wa tatu 1,000,000 wa nne 750,000 wakati wa tano atajitwalia Sh. 500,000 huku wale wa sita hadi kumi wakiondoka na Sh. 300,000 kila mmoja.

 

Mbio za Kilomita 10 mshindi atajitwalia kitita cha Sh. 1,000,000 wa pili Sh. 750,000 wa tatu Sh. 500.000 wa nne Sh. 250,000 wakati wa tano atajishindia Sh. 200,000 wakati wa sita hadi kumi wakijipoza na Sh. 100,000.

 

Kwa upande wa mbio za kujifurahisha za Kilomita 5, washiriki wote watakaofanikiwa kumaliza watajipatia medali.

 

Ada kujisajili ni Sh. 25,000 ambapo usajili unaendelea katika matawi ya NBC, Shoppers Plaza jijini Dodoma na Mlimani City Dar es Salaam. Kila atakayejisajili pia atapata fulana maalumu ya kukimbilia.

 

Mbali na kujenga afya na kupromote mchezo wa Riadha, NBC Marathon inalenga kusaidia jamii yenye uhitaji, ambapo kwa mwaka huu mapato yote yatakayopatikana kupitia usajili yatapelekwa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road kusaidia akina mama wanaosumbuliwa na kansa ya shingo ya kizazi.

No comments:

Post a Comment

Pages