NA DANSON KAIJAGE, DODOMA
KANISA
la TAG Upendo Revival Christian Center Dodoma imeazimisha siku ya
kuzaliwa kwa Yesu Kristo kwa kushiriki chakula cha mchana na
wajane,yatima na watoto wanaotoka katika mazingira magumu.
Mchungaji
kiongozi wa kanisa hilo Dk Salum Vangasiti akizungumza na waumini
waliokuwepo katika ibada ya maalum kushiriki chakula cha pamoja na
yatima ,wajane na wale wanaotoka katika familia zenye uhitaji.
Mchungaji
huyo amesema ni muhimu kushirikiana na makundi mbalimbali hususani
katika siku muhimu kama kumbukizi ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo au
mwakampa ili jamii hiyo nayo ijione kuwa ni sehemu ya furaha.
Mchungaji
Dk.Salum amesema kanisa linawajibu wa kuhakikisha linafanya kazi kubwa
katika jamii ambayo ni ya kuokoa roho za watu na kuhakikisha
wanabarikiwa na kimwili.
"Kanisa
letu limeona kuwa ni vyema siku kama ya leo ya kukumbuka kuzaliwa kwa
Yesu Kristo ni vyema kufanya ibada ya kushirikiana na makundi mbalimbali
ya watu wasiojiweza,yatima na wajane.
"
Yesu Kristo anasema kuwa ibada iliyo njema ni pamoja na kuwajali watu
wenye uhitaji kama tulivyofanya sisi licha ya kushirikia nao chakula cha
pamoja bila kujali itikaji za dini pia tunatoa zawadi mbalimbali
zikiwemo fedha"amesema Mchungaji Dk.Salum.
Akizungumzia
habari ya amani ya nchi amewakata viongozi wote wa kisiasa,kidini
pamoja na taasisi mbalimbali kufanya kazi zao kwa uadilifu sambamba na
kutoa haki kwa kila mmoja.
"Ili
uweze kuwa viongozi mzuri ni lazima ufanye kazi kwa misingi ya utii wa
Kimungu pamoja na kujiondoa katika masuala ambayo yanaweza kukunyima
ujasiri wa kutoa maamuzi.
"
Kiongozi ambaye hatendi haki wala atoe maamuzi ya haki kamwe hawezi
kujisimamia na hawezi kuwa na ujasiri wa kutoa haki kwa wale ambao
wanaonewa"amesisitiza Mchungaji.Dk.Salum.
Akizungumzia
viongozi wa kisiasa amewataka kuhakikisha wanatunza amani ya nchi
pamoja na kufanya kazi kwa masilahi mapana kwa taifa na wananchi wake.
No comments:
Post a Comment