HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 30, 2020

Milioni 398 za COSTECH zajenga maabara ya kudhibiti ubora wa chanjo za mifugo- TVLI-Kibaha


Mkuu wa Kituo cha TVLI-Kibaha Dk. Stela Bitanyi akionyesha nanna bora ya kuhifadhi sampuli za chanjo za mifugo.

 

Mkurugenzi wakituo cha TVLI-Kibabha akizungumza kuhusu kituo hicho kinavyofanya kazi.


 

NA MWANDISHI WETU

 

SERIKALI kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imetoa kiasi cha Sh.Milioni 398 ili kujenga maabara ya kudhibiti ubora wa chanjo.

 

Fedha zilitolewa kwa Taasisi ya Utafiti wa Chanjo za Mifugo Tanzania (TVLI) ilitopo wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani ambayo iko  chini ya Wakala wa Maabara ya Utafiti wa Mifugo (TVLA) iliyoanzishwa mwaka 2012 ikiwa na jukumu la kuhakikisha inadhibiti magonjwa ya mifugo yaliyopewa kipaumbele nchini.

 

Akizungumzia matumizi ya fedha hizo wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani jana Meneja wa TVLI-Kibaha, Dkt Stella Bitanyi amesema mwaka 2018, TVLI-Kibaha  ilipata ruzuku kutoka serikalini kupitia Tume yab Taifa ya Sayansi na Teknolojia COSTECH) kiasi cha Sh.Milioni 398.8 kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali zilizokuwa zinaikuwa taasisi hiyo.

 

Amesema baada ya kupokea feeha hizo waliamua kujenga Maabara ambayo hadi sasa  imeshakamilika na kuanza kutumika.

 

“TVLI ipo kwenye mazungumzo ya kupima ubora wa chanjo zitakazozalishwa na viwanda binafsi wakianza na kiwanda cha Hester Biosciences International kinachoendelea kujengwa mjini Kibaha”

 

“Katika utekelezaji wa majukumu yake TVLI imekuwa ikikumbana na changamoto ya upungufu wa vifaa kwa maabara yenye ubora wa kusaidia udhibiti wa chanjo za magonjwa ya kimkakati, kwa miaka ya hivi karibuni”Amesema Dkt.Bitanyi

 

 Dkt.Bitanyi ameongeza kuwan taasisi ilikuwa inazalisha chanjo mbili lakini tangu kukamilika kwa maabara hiyo kwa sasa imefikisha chanjo sita huku kukiwa na mkakati wa kufikisha chanjo nane hadi 13 ifikapo mwaka 2022.

 

“Kwa sasa maabara imekamilika ina vifaa vyote muhimu vya kupima na kuthibitisha ubora wa chanjo pamoja na uteketezaji wa uchafu utakaozalishwa na maabara (laboratory waste).

 

“Hii imeongeza tija katika vipimo vya chanjo kwa kuzingatia ubora kabla hazijapelekwa kwa wafugaji pamoja na wadau wengine wenye uhitaji huo”

 

“Uwepo wa maabara hii umechangia kuongezeka kwa uzalishaji wa chanjo kutoka aina tatu sita ambazo ni chanjo ya: Mdondo wa kuku, Kimeta, Chambavu, Homa ya mapafu ya Ng’ombe, Mchanganyiko (Kimeta na Chambavu) pamoja na Ugonjwa wa kutupa mimba kwa ng’ombe”Amesema Dkt.Bitanyi

 

Taasisi ya TVLI inatengeneza makundi ya aina mbili za chanjo ambayo  ni chanjo dhidi ya bakteria na la pili ni chanjo dhidi ya virusi ambazo zote ubora wake huthibitishwa katika maabara hiyo.

 

Kwa kutambua umuhimu wa chanjo ya mifugo na kuongezeka kwa idadi ya chanjo zinazozalishwa ili kuthibitisha ubora wake, kabla ya kuzipeleka kwa wakulima, COSTECH ilitoa ruzuku iliyofanikisha ujenzi wa maabara inayosaidia kupata chanjo zenye ubora.

Mradi huo umesaidia kuongeza tija na ufanisi kwa wafanyakazi, wakulima, wazalishaji na waagizaji wa chanjo nchini, hatimaye kukuza pato la Taifa, kuimariisha afya (lishe bora) na kuongeza wigo wa biashara. 

No comments:

Post a Comment

Pages