wa Serikali Dodoma.
Mhandisi
Sanga amefanya mazungumzo na Balozi Christian aliyeambatana na baadhi
ya wafanyabiashara wenye makampuni makubwa kutoka Austria, kwa lengo la
kuangalia namna ya kushirikiana katika sekta ya maji.
“Kimsingi,
tunaangalia sehemu ambazo tunaweza kushirikiana nao katika uwekezaji wa
miundombinu ya maji, kupitia ugeni huo tunatafuta pesa za kujenga
miradi ya maji,” Mhandisi Sanga, amesema.
Naye
balozi Dkt. Christan Fellner amesema kwamba anamshukuru sana Balozi wa
Tanzania nchini Kenya Balozi John Simbachawene kwa kuandaa na kuwezesha
ujumbe wa wafanyabiashara hao kufika Tanzania na kufanikisha mazungumzo hayo.
Naye, Balozi Simbachawene amesema makampuni hayo 13 ya kimataifa kutoka Austria yamevutiwa katika masuala ya uwekezaji hapa nchini hususan maendeleo ya kuboresha miundombinu mbalimbali.
Mazungumzo yakiendelea baina ya Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga na ugeni uliomtembea.
Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Austria nchini Tanzania Dkt. Christian Fellner, na wafanyabiashara kutoka Austria alioambatana
nao.
No comments:
Post a Comment