HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 16, 2020

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar atambelea Wagonjwa

 


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha ACT wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad amefanya ziara maalum ya kuwaona na kuwafariji wagonjwa katika kisiwa cha Unguja.

Makamu wa kwanza aliaza zara yake hiyo katika mtaa wa kwa haji Tumbo mjini Unguja ambapo alionana na mjumbe wa Ngome ya wazee Mkoa Mjini Kichama Masoud Khamis Masoud ambaye anasumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu.

“Namuomba mwenyezi mungu akujaalie Uzima wa haraka ili urudi katika shuhuli zako za kichama na kuhudumia familia yako” alisema Maalim Seif.

Sambamba na Masoud pia Makamu wa Kwanza aliweza kuwafariji Mzee Shambuli Hamad Makame wa Chuini ambaye alipatwa maradhi ya Baridi Pamoja Hashirini Othmani Hashiri wa kijiji cha Kitundu.

Akiwa katika ziara yake hiyo Maalim Seif alikuwa ameambatana na katibu wa habari na Uenezi wa chama hicho Salim Bimani pamoja na wajumbe wengine.

Akizungumza mara bada ya kumaliza ziara hiyo,maalim aliwatakiya afya njema watendaji hao wa chama na kuwaombea kwa Mungu kurudi katika shughuli za utekelezaji wa majukumu ya kisiasa na ya kijamii kwa ujumla.

 

‘’Ziara niliyoifanya ni kwa ajili a kuwajuliya haliviongozi wetu wa chama kupona haraka na kurudi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kisiasa na kichama pamoja na kijamii kwa ujumla’’alisema maalim.

Pia wagonjwa wote hao walimpongeza Maalim Seif na Chama chake kwa kukubali kushiriki katika serikali ya Uboja wa Kitaifa na kueleza kuwa ni matumaini yao maendeleo ya haraka yataweza kupatikana Visiwani zanzibar.



No comments:

Post a Comment

Pages