HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 16, 2020

UME YA MADINI YAENDELEA KUVUKA LENGO UKUSANYAJI WA MADUHULI Yakusanya shilingi bilioni 260 sawa na asilimia 118 ndani ya kipindi cha miezi mitano kwa mwaka wa fedha 2020-2021


Mwenyekiti wa Tume ya Madini Profesa Idris Kikula amesema kuwa kati ya kipindi cha mwezi Julai hadi Novemba, 2020 ndani ya mwaka wa fedha 2020-2021 Tume ya Madini kupitia Ofisi za Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa imekusanya kiasi cha shilingi bilioni 260 ikiwa ni asilimia 118 ya kipindi husika.

Profesa Kikula ameyasema hayo leo tarehe 15 Desemba, 2020 jijini Dodoma katika kikao kazi cha Tume ya Madini ambacho kinakutanisha Wakurugenzi na Mameneja kutoka Makao Makuu ya Tume ya Madini pamoja na Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa na Maafisa Bajeti chenye lengo la kujifunza namna bora ya kuandaa bajeti kwa mwaka wa fedha 2021-2022.

Amesema kuwa awali katika mwaka wa fedha 2020-2021 Tume ya Madini ilipangiwa lengo la kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 526 na kufafanua kuwa ndani ya kipindi cha mwezi Julai hadi Novemba, 2020 Tume ya Madini imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 260 ambayo ni sawa na asilimia 118 ya kipindi husika.

“Nipende kuchukua nafasi hii kuwapongeza Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa kwa kazi nzuri sana ya ukusanyaji wa maduhuli, ninawataka kuongeza kasi ya ukusanyaji wa
maduhuli kwa ubunifu wa hali ya juu ili kuhakikisha Sekta ya Madini inaendelea kuwa na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi,” amesema Profesa Kikula.

Ameendelea kusema kuwa watanzania wengi wana matarajio makubwa sana kwenye Sekta ya Madini hivyo ni vyema watendaji wa Tume ya Madini wakahakikisha
wanatimiza kiu ya watanzania.


Katika hatua nyingine Profesa Kikula amewataka maafisa madini wakazi wa mikoa kuhakikisha hawawaonei haya watoroshaji wa madini na kusisitiza kuwa Tume ya Madini haitasita kuchukua hatua za kisheria kwa watu wanaojihusisha na vitendo vya utoroshaji wa madini nchini.

Wakati huohuo Profesa Kikula amepongeza kazi kubwa inayofanywa na Kurugenzi ya Ukaguzi wa Migodi na Mazingira ya kuelimisha wachimbaji wadogo wa madini na kuwataka kuendelea kutoa mafunzo hayo katika mikoa mingine nchini.

Aidha, Profesa Kikula amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kumteua kwa mara nyingine Waziri wa Madini, Doto Biteko na aliyekuwa Katibu
Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya kuwa Naibu Waziri wa Madini.

Naye Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba amemhakikishia Profesa Kikula kuwa watumishi wa Tume ya Madini wanaunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kwenye usimamizi wa rasilimali za madini na kusisitiza kuwa watahakikisha Sekta ya Madini inasimamiwa kwa uadilifu na ubunifu wa hali ya juu na kuchochea
ukuaji wa Sekta nyingine nchini.

No comments:

Post a Comment

Pages