Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Ocode Joseph Jakson katikati akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa manispaa ya Ubungo ambapo waliweza kuhudhulia kwa lengo la kujionea mwenendo mzima wa program hiyo ambayo iliwajumuisha na wanafunzi mbali mbali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ocode (katikati) mwenye fulana nyekundi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi mbali mbali wa serikali pamoja na wanafunzi ambao waliweza kufanya vizuri katika mambo mbali mbali ikiwemo katika michezo ya mpira wa miguu. (PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU).
VICTOR MASANGU, KIBAMBA
KATIKA kuunga mkono juhudi za serikali katika kupambana na vita dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto wa kike na wakume Shirika lisilokuwa la kiserikali la Organization for Community Development (OCODE) limekuja na mpango wa kampeni maalumu ambayo itawasaidia wanafunzi wa shule za awali na msingi zilizopo katika manispaa ya Ubungo lengo ikiwa ni kuwajengea uwezo katika kupinga vitendo vya ukatili.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi mtendaji wa Shirika hilo la (OCODE) Joseph Jakson wakati wa sherehe za ufunguzi wa kampeni maalumu ya siku 16 kwa ajili ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa watoto wa kike zilizoandaliwa na shirika hilo kwa lengo la kuelimisha jamii kuhusiana na vitendo vya ukatili ambayo imefanyika katika kata ya kibamba manispaa ya ubungo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi huyo alibainisha kuwa shirika hilo ambalo lilianzishwa mnamo mwaka 1999 kwa sasa linatekeleza miradi mbali mbali ya vijana lengo lake kubwa ikiwa ni kusaidia na kuiwezesha jamii kuweza kutambua umuhimu wa elimu bora kuanzia ngazi ya awali pamoja na ile ya msingi kwa watoto na kuwajengea vijana uwezo katika kuboresha masiha yao.
“Shirika letu la Ocode kwa kushirikiana na wadau pamoja na viongozi wa serikali kutoka manispaa ya Ubungo tumeona tumekuwa tukishirikiana bega kwa bega katika miradi yetu mbali mbali lakini kwa wakati huu tupo kwa ajili ya kuungana kwa pamoja kwa ajili ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ambayo yanatarajia kufanyika kidunia disemba 10 mwaka huu,”alisema Mkurugenzi huyo.
Kadhalika aliongeza wameamua kuzitumia siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa lengo la kuweza kutoa elimu mbali mbali kwa vijana pamoja na wanafunzi kuhusiana na vitendo vya ukatili ili kuweza kuona namna gani ya kuweza kuwapa fursa ya kujitambua na hatimaye kuendelea kuishi kwa misingi ya kupatiwa haki bila uonevu wowote.
Kwa upande wake mkurugenzi wa kampuni ya ushauri wa masuala ya afya Dr. Cecilia Mkafu ambaye alikuwa mgeni rami katika halfa hiyo amebainisha kuwa katika kukabiliana na kujiepusha na unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto wa kike wanapaswa kuhakikisha wanajiamini na kujitambua pamoja na kupatiwa elimu ili waweze kutambua haki zao za msingi.
“Natambua kuna siku 16 za ukatili wa kijinisia ambazo uwa zinaazimishwa kila mwaka kwa hivyo mimi kwa upande wake nalipongeza shirika la Ocode kwa kuweza kutenga siku hii kwa ajili ya kufanya kampeni maalumu ambayo imewashirikisha wanafunzi mbali mbali wa manispaa ya ubungo yote haya ni kwa lengo la kushiriki na kujifunza mambo mbali mbali ya kupinga unyanyasaji wa kijinsia.
Naye mmoja wa walimu waliohudhulia hafla hiyo Amina Muchumu amewaomba wazazi na walezi kuhakikisha kwamba wanaondokana na wimbi la kuwafanyia vitendo vya ukatili na unyanyasaji ya kijinsia watoto wao na badala yake watilie mkazo zaidi katika kuwapeleka shule na kuimba serikali kuwachukulia hatua kali kwa wale watakaobainika wanavunja sheria.
SHIRIKA la Organization for Community Development (OCODE) ambalo limeanishwa mwaka 1999 limekuwa likishirikiana na serikali kwa hali na mali katika kuisaidia jamii katika masuala ya kuleta maendeleo ikiwemo kuwajengea uwezo vijana pamoja na wanafunzi wa shule za awali na msingi waweze kujitambua katika mambo ya kimaendeleo.
No comments:
Post a Comment