Mkuu
wa Biashara ya Kadi wa Benki ya NMB - Philbert Casmir akionyesha baadhi
ya zawadi zinazotolewa kwa wateja katika kampeni ya Mastabata Siyo
Kikawaida zikiwemo; Friji, TV Simu na vinginevyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NMB wakifurahia 'NMB Friday'.
Benki
ya NMB imeendelea kuhakikisha wateja wao wanafurahia na kufaidika na
huduma zao ikiwemo kutoa elimu juu ya umuhimu wa matumizi ya mifumo ya
digitali katika kupata huduma kwa usalama wa fedha zao.
Akifafanua
zaidi, Mkuu wa Biashara ya Kadi wa Benki ya NMB- Philbert Casmir
amesema kuwa, Benki hiyo imekuja kivingine Msimu huu wa Sikukuu kwa
kuhakikisha wateja wao wanafaidika kupitia kampeni zao za 'NMB Fri-Yay'
na MastaBata Sio Kikawaida.
“NMB inatambua kila
siku lazima wateja wetu wafanye huduma mbalimbali ikiwemo kupata
chakula, kujaza mafuta katika magari yao na kufurahia, na kupitia 'NMB
Fri-yay' kila ijumaa ya mwisho wa mwezi kila anaelipa kupitia kadi zao
za NMB Mastercard na Mastercard QR atapata punguzo hadi la asilimia 15,
wakinunua bidhaa katika vituo vya mafuta vilivyoainishwa na hiyo ni
pamoja na sehemu za vyakula na maeneo ya starehe ambayo tumeingia ubia
na wafanyabiashara katika Mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Moshi, Dodoma,
Mwanza na Zanzibar.
Tunaimani kampeni hizi zitawapeleka wateja katika
njia ya kidigitali na kutunza miamala yao ya kibenki."
Amesema
hiyo yote ni katika kuwatoa wateja katika mfumo wa matumizi ya fedha
taslimu katika kufanya manunuzi na kutumia mfumo wa kadi katika kufanya
malipo ya huduma njia ambayo ni rahisi na salama zaidi.
Ameeleza
kuwa, katika msimu huu wa sikukuu, wanahakikisha wateja wao wanafurahia
sikukuu za mwisho wa mwaka kwa kununua bidhaa na kutembelea sehemu
mbalimbali kupitia kampeni ya 'MastaBata sio kikawaida' kampeni
iliyoifanya benki hiyo kuendelea kuwa kinara kwa kuwazawadia wateja wao.
"Kupitia
kampeni hii tunatoa zawadi kwa wateja wetu pamoja na kutoa elimu ya
kuacha matumizi za fedha taslimu njia ambayo ni gharama na si salama na
kugeukia matumizi ya kadi katika kufanya huduma." Amesema Philbert.
Ameeleza
kuwa kampeni ya 'MastaBata Sio Kikawaida' ni ya muda wa miezi mitatu
ikiwa na zawadi za wiki, mwezi na zawadi za mshindi wa jumla. Nayo pia
ikiwalenga wanaotumia kadi za NMB Mastacard na Mastacard QR kufanya
manunuzi.
"Katika zawadi za wiki, kila wiki
kuna washindi 40 wanajishindia laki moja kila mmoja, zawadi za mwezi ni
simu ya kisasa aina ya Samsung Galaxy note 20 na zawadi kubwa ya mwisho
ya kumalizia kampeni ni kuwapeleka wateja wetu kutembelea vivutio
mbalimbali zikiwemo mbuga za wanyama za Serengeti, Ngorongoro na Visiwa
vya karafuu visiwani Zanzibar." Amesema.
Aidha amesema kuwa hiyo ni katika kudumisha utalii wa ndani wateja watapata huduma za hadhi ya nyota tano.
"Na
tumeiita 'MastaBata Sio Kikawaida' kwa sababu mteja mwingine anaweza
asisafiri au tayari ameshatembelea maeneo ya vivutio basi atakuwa na
machaguo, gharama ileile ya kusafiri atachagua zawadi nyingine nyingi
zikiwemo Televisheni ya kisasa, jokofu, Microwave, Kompyuta mpakato na
simu za mkononi na hii yote ni katika kuwazawadia wateja wetu na kujenga
uelewa wa umuhimu wa kutumia kadi za NMB Mastercard na Mastercard QR
inayopatikana kupitia NMB Mkononi." Amesema.
NMB
ina wateja zaidi ya milioni tatu wenye kadi na inawasihi waendelee
kuzitumia ili waweze kunufaika na hizi ofa hasa msimu huu wa Sikukuu
lakini wajijengee mazoea ya kutotumia pesa taslimu (keshi).
No comments:
Post a Comment