HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 23, 2020

COSTECH yatoa Sh.Mil.500 kuwezesha miundombinu ya Utafiti TAFIRI-Rorya

 

Mkuu wa Kituo cha TARIRI-SOTA, Tausi Khitentya, akifafanua kuhusu  utendaji kazi wa kituo hicho baada ya kkamilika kwa majengo yaliyojengwa kwa ruzuku kutoka serikalini kupitia COSTECH.

Muonekano wa Jengo la Utawala la Kituo cha TAFIRI-SOTA-Rorya baada ya Ujenzi mpya kukamilika kutokana  ruzuku iliyotolewa na  serikali kupitia COSTECH
Mwakilishi wa kikundi cha Mcheo akiongea afisa kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia.
 


NA MWANDISHI WETU

 

 MKUU wa Kituo cha Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) katika Kijiji cha Sota wilayani Rorya Mkoa wa Mara  Tausi Khitentya anameishukuru Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia COSTECH) kwa kutoa zaidi ya  Sh.Milioni 500 zilitotumika kujenga majengo ya maabara.

 

Hata hivyo Khitentya anaiomba serikali pamoja na wadau wengine kuendelea kusaidia kuboresha miundombinu inayohitajika katika Kituo hicho ili kuongeza tija zaidi ya ufugaji samaki katika  Kanda ya Ziwa na Nchi kwa ujumla.

 

Anasema fedha hizo zimetumika katika kujenga majengo mawili ambayo yamewaondolea kero nyingi na kuwaongezea ari ya kufanya kazi kwani sasa ni rahisi kwao kupatikana kwa kuwa wananchi wanajua zilipo ofisi zao.

 

Anafafanua kuwa kwa sasa wana uhitaji wa nyumba za wafanyakazi pamoja na mlinzi.

 

“Jengo la maabara limekamilika na lipo tayari kufanya kazi wakati huo lile la utawala likiwa linatumika hivi sasa hivyo kuinufaisha taasisi, wafanyakazi wake, wafugaji na wadau wengine wa samaki.”anasema Khitentya.

 

Awali Mwaka  1980, Serikali ilianzisha Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI), ambapo mwaka 1988 ilianzisha mradi wa kusimamia na kuratibu masuala yanayohusu samakali aina ya Sangara katika Kijiji cha Sota wilayani Rorya, mkoani Mara mwaka.

 

Mradi huo ulipokamilika, shughuli zake zikaendelezwa kama Kituo kidogo cha TAFIRI.

 

Mradi huo ulihusisha uchimbaji mabwawa tisa ambayo bado yanatumika kufundishia wafugaji, kuzalisha vifaranga na kufanikisha utafiti wa samaki.

 

Hata hivyo Mwaka 2004 kituo hicho kilianzisha teknolojia ya ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba ambapo mwaka 2007 kilianza rasmi kutoa mafunzo kwa wananchi juu ya  teknolojia hiyo ambayo sasa wanaitumia kufuga samaki kwenye ziwa Victoria.

 

TAFIRI katika Kijiji hicho cha Sota haikuwa na majengo ya ofisi hivyo kulazimika kupanga kwenye nyumba za watu binafsi.

 

Mwaka 2018 kituo hicho kidogo kiliomba ufadhili wa kiasi cha shilingi 532.1 kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) ili kijengewe jengo la kuangulia vifaranga, jengo la utawala pamoja na maabara ya utafiti.

 

Majengo ya kituo hicho ambayo yameshakamilika hadi sasa ni yale ya maabara na utawala ingawa hayana vifaa muhimu.  

 

Maabara hiyo inatarajiwa kupima ubora wa chakula cha samaki, magonjwa ya samaki, udongo, maji, mifumo ya samaki wenyewe na mimeamaji huku jengo la utawala likifanikisha shughuli nyingine muhimu.

No comments:

Post a Comment

Pages