HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 27, 2020

NMB YATOA MSAADA HOSPITALI YA WILAYA MBULU

 

Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Dk. Chelestino Mofuga (kushoto), akipokea msaada wa magodoro na vitanda kutoka kwa Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mbulu mkoani Manyara, Adamu Mwaisumo, NMB walitoa msaada wa mashuka 25, vitanda 8 na magondoro yake vyote vikiwa na thamani ya Sh. Milioni tano kwa jili ya hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara, iliyopo eneo la  Dongombesh. (Na Mpiga Picha Wetu).

Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Dk. Chelestino Mofuga (kushoto), akiwa na Mkurungenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Hatson Kamoga (wa pili kushoto), pamoja na Mbunge wa Jimbo hilo, Flatei Massay (wa tatu kushoto), wakipokea msaada wa mashuka 25 na vitanda 8 na magodoro yake kutoka kwa Meneja wa NMB Tawi la Mbulu, Adamu Mwaisumo (kulia). Benki ya NMB ilikabidhi vifaa hivyo mwishoni mwa wiki kwa ajili ya hospitali ya  Halmashauri ya wilaya ya Mbulu vyenye thamani ya Sh Milioni tano. 
 

 

Mkuu  wa Wilaya ya Mbulu, Dk. Chelestino Mofuga amewataka wananchi kuziunga mkono Taasisi za kifedha zinazoshirikiana nao katika kuihudumia jamaii

Dk. Mofuga alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki kwenye hotuba yake alipokuwa akipokea msaada wa mshuka ,vitanda na magodoro  yaliyotolewa na Benki ya NMB kwa ajili hospitali mpya ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara iliyopo eneo la Dongobesh .

Mkuu huyo wa Wilaya  aliwataka wananchi kuziunga mkono taasisi  zinazotoa huduma za kifedha  ambazo zipo tayari kuendelea  kushirikiana na Jamii kwa kutoa misaada .

“Na hapa naomba niwe mkweli tangu nimekuja hapa nasikia benki ya  Nmb wanakabidhi misaada maeneo mbalimbali wilayani hapa , na leo nimepokea  msaada mwingine  hawa  ndio  watu mnaotakiwa kuungwa mkono kwa sababu wanarudisha faida kwenye jaami yetu na tunaiona ”alisema.

Kadhalika alisema benki ya NMB imekuwa ni taasisi pekee ya kifedha inayotoa huduma za kifedha kwa  kuwafikia wananchi waliopo maeneo ya vijijini bila kujali faida kama wengine wanaonga’ng’ania mijini.

Aidha aliwataka wananchi kutumia taasisi za kifedaha katika kuhifadhi fedha zao ili kuepuka kupata hasara wakati wa majanga ya moto au wizi kwenye nyumba zao .

Hata hivyo Mkuu huyo wa Wilaya  aliahidi kuwa balozi wa benki ya Nmb Nchini kwa kuisemea kutokana na misaada inayotolewa katika maeneo mbalimbali inavyoigusa jamii.

Naye Meneja wa Nmb Tawi la Mbulu ,Adamu Mwaisumo alisema  benki hiyo imekabidhi mashuka 25,magodoro nane na vitanda nane kwa ajili ya wodi za kawaida na akinamama kujifungulia  ya hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu iliyopo MKoani Manyara

Mwaisumo alibainisha kuwa msaada huo wa vifaa hivyo vyote unathamani ya shilingi milioni tano ambazo zimetokana na asilimia 1 ya faida baada ya kodi inayotengwa na NMB kila Mwaka katika kuirudisha kwenye jamii.

Alisema benki hiyo inasaidia jamii katika sekta ya elimu kwa kuchangia madawati,viti na meza pamoja na kusaidia kuezeka majengo mapya ya shule au nyumba za waalimu

Aliongeza kuwa eneo lingine ambalo NMB inasaidia jamii kuwa ni sekta ya afya kwa kutoa vifaa tiba,mashuka,magodoro,vitanda vya kawaida na akinamama  kujifungulia

Pia alisema lengo la msaada huo wa Nmb ni kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli katika kuihudumia jamii.

Kwa upande wake Mkurungenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mbulu ,Hardson Kamoga alisema hospitali hiyo mpya inakabiliwa na changamoto ya vifaa hivyo anaziomba  Taasisi zingine kujitokeza kusaidia.

Aliwashukuru benki ya Nmb kwa msaada uliotolewa na kuahidi kuvitunza vifaa hivyo vilivyotolewa ili kuendelea kuwasidia wananchi wote wanaofika kupata huduma hapo .

Alibainisha kuwa hospitali hiyo mpya imeanza kutoa huduma za awali lakini bado huduma hivyo wananchi wafike kupata huduma za kiafya.

No comments:

Post a Comment

Pages