Wadau
wa ukatili wa kijinsia kesho Disemba 5, 23020 watazindua
mapungufu yaliyomo kwenye sheria zinazohusiana na ukatili wa kijinsia
ikiwa ni sehemu ya vuguvugu la kupinga ukatili wa kijinsia.
Kongamano
hilo ni mfululizo wa kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia
na litafanyika katika ukumbi wa Watu wenye ulemavu, Kikwajuni Weles,
Zanzibar.
Wadau hao
wakiwemo Chama cha Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA), Jumuia wa
Wanawake Wenye Ulemavu (JUWAUZA), Mtandao wa Kijinsia Zanzibar (ZGC) na
Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Zanzibar (TAMWA ZNZ) walipitia
sheria saba zinazohusiana na masuala hayo na kukuta tofauti na kukizana
jambo ambalo linapelekea kukwama kwa kesi hizo katika vyombo vya sheria
ama kupata hukumu ndogo.
Sheria
hizo ni pamoja na sheria ya Adhabu No 7 ya mwaka 2018, sheria ushahidi
no 9 ya 2017, sheria ya mtoto no 6 ya 2011, sheria ya elimu No 6 ya 1982
sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai No. 6 ya 2018, sheria ya Mahakama
ya kadhi No 9, 2017, sheria ya kumlinda mwari na mjane No 4 ya 2005.
Kongamano
hilo litatoa nafasi kwa washiriki kujadili mapendekezo na nini
kifanyike katika hatua za kuboresha sheria na utendaji wa taasisi husika
katika kupunguza wingu la ukatili wa kijinsia.
Vitendo
vya ukatili wa kijinsia vinaendelea kushamiri na bado kwa mujibu wa
takwimu watu wanaopata hukumu ni kidogo sana ambapo kwa mujibu wa
taarifa ya Jeshi la Polisi zinaonyesha kuwa kuanzia Januari 2019 hadi
Agosti mwaka huu, malalamiko 821 ya ubakaji na ulawiti
yameripotiwa lakini ni kesi nne tu hadi sasa ndizo zilizopatiwa hatia, sawa na asilimia 0.73% .
Hali
hiyo inaonesha mapungufu makubwa katika sheria pamoja na utekelekezaji
wake ambapo hutoa mwanya kwa wabakaji kukimbia makosa yao na hivyo
kuendeleza tabia hiyo ovu.
Maadhaimisho
ya Siku 16 za kumpinga ukatili wa kijnsia hufanyika kila mwaka kuanzia
tarehe 25 Novemba hadi tarehe 10 Desemba, siku ya kilele chake.
No comments:
Post a Comment