Mtaribu wa Mnyororo wa Thamani wa Mazao ya Misitu (FORVAC), Emmanuel
Msoffe akiandaa mche wa Msaji mbele ya waandishi ili ukapandwe.
NA SULEIMAN MSUYA
WATANZANIA
wameshauriwa kutunza na kuendeleza rasilima misitu ili kuwa na uhakika
wa kupata mvua na kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi.
Aidha
wameshauriwa kupanda miti aina ya misaji ambayo inafaa kibiashara huku
wakijihusisha na shughuli nyingine za kujipatia kipato.
Ushauri
huo umetolewa na Mratibu wa Program ya Myororo wa Thamani wa Mazao ya
Misitu (FORVAC) Emmanuel Msoffe wakati akizungumza na wananchi wa kijiji
cha Liuli na Nkalachi wilayani Nyasa mkoani Ruvuma ambao wanatekeleza
mradi wa upandaji miti ya misaji kijijini hapo.
Msoffe
aliambatana na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali kujionea
namna miradi ya Usimamizi Shirikishi wa Misitu ya Jamii (USMJ)
inavyotelezwa kwenye vijiji ambapo ziara ilianzia mkoani Lindi na
kuishia wilayani Nyasa mkoani Ruvuma.
Amesema
program ya FORVAC inatekelezwa na Idara ya Misitu na Nyuki chini ya
ufadhili wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Finland na Wizara ya Maliasili na
Utalii ya Tanzania.
Tanzania ina hekta milioni 48.1 za misitu lakini kutokana na ukataji miti hekta 469,000 zinaisha kwa kukatwa kila mwaka.
Msoffe amewataka wananchi wenye misitu ya asili popote Tanzania kuitunza huku wakiendelea na upandaji wa miti.
"Hapa
Liuli mmeonesha mfano wa kuendeleza misitu kwa kutunza Mlima Livingston
lakini niwapongeze kwa kuamua kupanda miti ya misaji ambayo ni fursa
kwa vizazi vijavyo," amesema.
Mratibu
amesema uhakika wa kuwepo misitu utakuwa endelevu kwa wanavijiji
kuendelea kupanda miti ya kibiashara kama misaji inayokubali eneo hilo.
Amesema
utafiti wao umebaini kuwepo kwa mapungufu ya kiusimamizi ndio sababu ya
uharibifu wa misitu hivyo kuishauri Serikali kutafuta na kutumia fursa
zilizopo.
Ameitaka jamii
kuondokana na hofu ya muda mrefu wa kusubiria kuvuna bali wajionee
huruma kwa sasa kurudi mabadiliko ya tabia nchi.
Mratibu huyo amesema wataendelea kuhamasisha jamii umuhimu wa kutunza misitu na vyanzo vya maji.
Kwa
upamde wake Msimamizi wa Mtaalam wa Misitu wa FORVAC, Alex Njahani
amesema uendelevu wa misitu ya vijiji na ile ya Serikali utachangiwa na
ushirikiano wa wadau wote.
Njahani amesema program hiyo imeweza kutoa matoe chanya kwa Semina elekezi kwa vikundi ambavyo vinajihusisha na lengo husika.
"Sisi tumekuwa tunashirikiana na wadau kuhakikisha sekta ya misitu inakuwa na tija kuanzia ngazi ya kijiji hadi taifa," amesema.
Mtaalam
huyo amesema FORVAC inatekeleza program hiyo kwenye wilaya 12 ambazo ni
Nyasa, Mbinga, Namtumbo, Songea na Tunduru zilizopo Kongani ya Ruvuma.
Amesema wilaya zingine ni Liwale, Ruangwa, Nachingwea Kongani ya Lindi, Handeni, Kilindi, Mpwapwa na Kiteto Kongani ya Tanga.
Njahani amesema matarajio yao ni kuona wanavijiji wanaozungukwa na misitu ya vijiji wananufaika nayo kupitia dhana ya USMJ.
No comments:
Post a Comment