HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 05, 2021

ASKOFU AHIMIZA MSAMAHA

NA DANSON KAIJAGE,DODOMA

 

ASKOFU wa Kanisa  la  The Potter's House Tanzania, Ruth Kusenha, amewahimiza watanzania kuwa na tabia ya kusameheana na kujisamehe wenyewe ili kujenga taifa lenye afya ya hofu ya Kimungu.


Ikiwa ni sehemu ya salamu za mwaka mpya kwa watanzania wote nchini askofu Ruth amesema kuwa ili kuwa na taifa lenye watu makini na wenye hofu ya Mungu ni lazima wajue umuhimu wa kuwasamehe waliowakosea na kujisamehe wenyewe.


Kiongozi huyo wa Kiroho amesema pamoja na mambo mengine taifa linatakiwa kujengwa kwa misingi ya upendo,ushirikiano pamoja na kuaminiana ikiwa ni pamoja kila mtu kutambua nafasi yake na umuhimu alionao.


"Mwaka 2021 uwe mwaka wa tofauti kwa watu wote jambo kubwa watanzania wajenge zaidi tabia ya kupendana,kuaminiana na kusameheana na kijisamehe.


" Ipo tabia ya baadhi ya watu wanaweza kusamehe lakini wao hawajui jinsi ya kujisamehe,wapo watu ambao hawataki kusamehe wala kusamehewa.


"Ninaposema wapo watu wanaweza kusamehe lakini hawawezi kujisamehe namaanisa nini mfano mimi nakusamehe wewe na wewe unabarikiwa lakini kila kila ninapokuona nakuwa nakumbuka kuwa jambo hilo linaendelea kunitesa wakati wewe tayari huko huru tayari"ameeleza Askofu Ruth.


Akizungumzia mwaka 2021 amesema uwe mwaka wa mabadiliko kwa kila mmoja kwa kufanya kazi kwa bidii zaidi.


" Tunatakiwa kufanya kazi za mikono kwa bidii sana na tunatakiwa kufanya kazi ya Mungu kwa bidii sana kwani kwa sasa hakuna muda wa kupoteza katika mambo ambayo hayana maana.


"Hasa vijana wenye nguvu wanatakiwa kuhakikisha wanabadilisha maisha yao ya kimwili na Kiroho kwa kufanya kazi na kufanya hivyo ni kutimiza maandiko kwani tunaelekezwa na vitabu vitakatifu kufanya kazi" amesisitiza Askofu Ruth.

No comments:

Post a Comment

Pages