HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 05, 2021

MAJALIWA AZINDUA MELI YA MV. MBEYA II


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipozindua Meli ya MV. Mbeya II kwenye Bandari ya Mbamba Bay wilayani Nyasa, Januari 5, 2021. Wengine pichani ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania,Deusdedit Kakoko, Mbunge wa Nyasa Mhandisi Stella Manyanya, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme, Naibu Waziri wa Ujenzi, Godfrey Kasekenya,Mwenyekiti wa Bodi ya MNamlaka ya Bandari Tanzania, Ignas Rubaratuka na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Ruvuma, Odo Mwisho. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akibonyeza kitufe  kupiga king’ora kuashiria uzinduzi wa Meli ya MV. Mbeya II kwenye Bandari ya Mbamba Bay wilayani Nyasa, Januari 5, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka Nahodha Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, Abdullah Mwingamno kuhusu uendeshaji wa Meli ya MV. Mbeya II wakati alipozindua Meli hiyo kwenye Bandari ya Mbamba Bay wilayani Nyasa, Januari 5, 2021.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitumia kionambali wakati alipozindua Meli ya Mv. Mbeya II kwenye Bandari ya Mbamba Bay wilayani Nyasa, Januari 5, 2021. Wa pili kushoto ni Mkewe Mary na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoka  kwenye Meli ya MV Mbeya II baada ya kuizindua kwenye Bandari ya Mbamba Bay Januari 5, 2021.  Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi baada ya kuzindua Meli ya JMV. Mbeya II kwenye bandari ya Mbamba Bay wilayani Nyasa, Januari 5, 2021. Kulkia kwake ni Mkewe Mary. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Meli ya MV. Mbeya II ambayo imezinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Januari 5, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

No comments:

Post a Comment

Pages