WAZIRI
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa.
NA SULEIMAN MSUYA
WAZIRI
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa amesema
atatumia nafasi yake kutetea haki za waandishi wa habari nchini huku
akisisitiza uzalendo na utaifa kwa kada hiyo.
Kauli
ya Waziri Bashungwa inakuja baada ya kuwasikiliza waandishi
walioshiriki mjadala wa pamoja kuhusu changamoto wanazopitia katika
kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
Wakiwasilisha
maelezo yao waandishi walimueleza Waziri Bashungwa kuwa pamoja na wao
kuwa na sifa za kitaaluma asilimia 80 ya wamiliki wa vyombo vya habari
wahatoi mikataba ya ajira, wenye mikataba utekelezaji wake ni
wakusuasua, sheria za kazi hazizingatiwi.
Aidha
waandishi walimueleza waziri kuwa waandishi wengi wanafanya kazi kama
vibarua kwa muda mrefu huku wakidhibitiwa kama waajiriwa.
Akijibu
hoja hizo za waandishi Waziri Bashungwa amesema uamuzi wa kukutana na
waandishi ni kutoa fursa kueleza hali halisi ili ajue anaanzia wapi.
Amesema
sekta ya habari ni muhimu kwa maendeleo ya nchi hivyo ni jambo la aibu
na kusikitisha iwapo kuna haki zinakiukwa bila hatua kuchukuliwa.
"Nimewaita hapa ili tuelezane hali halisi mnayopitia ili sisi kama wizara tuweze kuchukua hatua stahiki," amesema.
Bashungwa
amesema haingii akilini watu wanafanya kazi hatarishi na wamesomea ila
hawana mikataba hivyo kuahidi kushirikiana Ofisi ya Waziri Mkuu Ajira na
wadau wengine ili muafaka uweze kupatikana kwa haraka.
Waziri
huyo amesema wizara ina jukumu la kutatua changamoto wanazopitia
waandishi kwa kuzungumza nao ili kuwa kitu kimoja kwani ni wadau muhimu
kwa nchi na wananchi.
Aidha,
amewataka wamiliki wa vyombo vya habari kuzingatia sheria ya kazi
inavyotaka katika kutekeleza mikataba ya wafanyakazi na kwamba
hawatosita kuchukua hatua za kisheria kwa mwajiri anayekiuka taratibu.
Halikadhalika
Waziri Bashungwa amemtaka Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuhakikisha baraza
la habari na bodi ya habari vinaundwa ili waandishi waweze kupata eneo
la kufikisha matatizo yao.
Pamoja
na kuahidi kutetea haki za waandishi Waziri Bashungwa amewataka
waandishi wajiendeleze kielimu ili kukidhi hitaji la Sheria ya Habari
namba 12 ya mwaka 2016 inayotaka sifa ya mwandishi wa habari awe na
elimu ya diploma.
Kwa
upande wake Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,
Abdallah Ulega amesisitiza uzalendo na utaifa kwa waandishi wa habari.
Ulega
amesema waandishi wanapaswa kuandika mazuri ambayo yanafanyika hapa
nchini ili yaweze kujulikana na kuvutia wawekezaji ikiwemo sekta ya
wanayoisimamia.
"Nyie ni
watu muhimu sana katika kusukuma gurudumu la maendeleo naomba mtumie
kalamu zenu kuyalezea mazuri yanayofanywa na Serikali inayoongozwa na
Rais John Magufuli.
Lakini
kwa umaalum zaidi sekta hii tunaomba muitangaze sana kwani ina kundi
kubwa ambalo linahitaji mchango wenu kwa mfano Januari 12, 2021
tunacheza na DRC Congo tunaomba mtangaze nachambua mchezo huo," amesema
Naibu Waziri Ulega.
No comments:
Post a Comment