Cheifu Lazaro Chihoma (kulia mwenye kofia nyekundu), akitoa maelekezo kwa baadhi ya watumishi wa serimali juu ya umuhimu wa Machifu na zana wanazozitumia.
NA DANSON KAIJAGE, DODOMA
BAADA ya serikali kuruhusu na kutambua umuhimu wa cheo cha uchifu Chiefu wa Iyumbu Bwimbwi Lazaro Chihoma amesema yeye na baraza lake wanajipanga kumpatia tuzo Rais John Magufuli kwa kutambua hilo.
Cheifu Chihoma akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma amesema kitendo cha Rais Magufuli kutambua cheo cha uchifu ni moja ya kurudisha heshima za uchifu Karina maeneo ambayo yanastahili.
Amesema kuwa kurudishwa cheo hicho kutasaidia kwa kiasi mila na destuli katika jamii na kupunguza mmomonyoko wa maadili ambao unajitokeza kwa kasi.
"Mimi nikiwa Chiefu Chihoma wa imaya ya Iyumbu Bwimbwi pamoja na baraza langu pamoja na machiefu wengine baada ya kuona kuwa serikali imetambua cheo cha uchifu tunafanya maandalizi ya kukutana na Rais John Magufuli angalau kwa dakika tano au kumi ili kuweza kumpa zawadi.
"Tunajipanga kukutana na mkuu wa nchi mwezi wa sita na tuzo ambayo tunatakiwa kpatia Mkuu wa nchi ni Ngao,Kiti pamoja na ng'ombe dume ikiwa ni moja ya zawadi ambazo utolewa na machiefu kwa watu waliofanya vizuri"ameeleza Chiefu Chihoma.
Katika hatua nyingine Chiefu Chihoma amewataka wale wote wenye sifa ya kuwa chifu wanatakiwa kufanya kazi na serikali kwa kuishauri serikali kwa faida ya jamii.
Amesema kazi kubwa ya Chiefu ni kuhakikisha maadili yanalindwa pamoja na kulinda utaratibu wote wa nchi na kuhimiza shughili za kimaendeleo kwa faida ya jamii.
"Kazi ya uchifu siyo kutoa adhabu tu au kuvaa mavazi ya kichiefu bali ni kuhakikisha anasimamia shughuli zote za kimaendeleo na kimaadili.
"Kutokana na mfumo wa serikali Machiefu wanatakiwa kukaa na serikali kwa lengo la kuishauli katika masuala ya kuboresha uongozi na wakati mwingine kuwajuza mambo ambayo yanaweza kutokea siku za mbeleni "amesema Chiefu Chihoma.
No comments:
Post a Comment