NA HAMIDA RAMADHANI
WAZIRI
wa Nchi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo
amewataka Wakuu wa Mikoa hapa Nchini kuwa walezi wa shule za ufundi ili
kufanya mabadiliko na mapinduzi makubwa ya viwanda.
Waziri
Jafo ameseyasema hayo leo Jijini hapa wakati alipokuwa akizungumza na
walimu wapya na Wakuu wa Mikoa kupitia njia ya Mtandao ambapo amewataka
walimu kuacha kujifungia na badala yake wawashirikishe mafundi mahili
waliopo mitaani ili kuleta Mapinduzi ya viwanda kwa wanafunzi na shule
zote za ufundi.
Waziri
Jafo amesema shule za ufundi kipindi cha awali zilipoteza hadhi yake na
hapakuwa na miundombinu wala rasilimali watu hali za shule hizo zilikuwa
mbaya.
"Shule za ufundi zinawaandaa Vijana kujifunza masuala ya ufundi hivyo basi niziagize Halmashauri zote zisimamaie miondombinu ya shule hizo na kuzikarabati kila wakati," amesema Waziri Jafo.
Aidha
amefafanua kwamba jumla ya Shilingi bilioni 16.34 zimetengwa na
Serikali kwa ajili ya ukarabati wa shule zote za ufundi ambapo pia jumla
ya walimu150 wameajiliwa ili kupelekwa katika shule hizo.
"Hivyo
basi Niwaagize walimu wote walioajiliwa waakikishe wanakwenda kufanya
kazi kwa bidii na umahiri katika taaluma hiyo ya ufundi hatutaki kusikia
habari za kununua Chaki na badala yake shule hizi za ufundi zitengeneze
Chaki," .
Na kuongeza
kusema kuwa " Haiwezekani hadi leo bado tunaagiza vijiti vya meno nchini
China hii ni aibu wakati tunamiti ya kutosha kwaajili ya kutengeneza
mbao," amesema Waziri Jafo.
No comments:
Post a Comment