Na Mwandshi Wetu
Serikali imetambua bunifu 1066 nchini na kuendeleza zingine 130 ili kuinua vipaji vya watanzania vitavyosaidia kutoa ajira na kukuza uchumi wa Taifa.
Kauli hiyo imetolewa juzi na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,Prof.James Mdoe wakati wa mahafali ya 12 ya Chuo cha Ufundi Arusha(ATC) ambapo jumla ya wahitimu 667 wamefuzu masomo yao katika ngazi ya Astashahada,Stashahada na Shahada.
Amesema kuanzia mwaka 2019 wizara ilianza kuibua na kuwatambua wabunifu na wagunduzi kwa kuendesha mashindano ya kitaifa ya Sayansi ,Teknolijia na Ubunifu(MAKISATU) na kuweza kutoa tuzo kwa wabunifu mahiri na kuwaendeleza ili kuweza kubiasharisha bunifu zao.
“Hadi sasa serikali imeshatambua bunifu 1066 nchini na kuendeleza bunifu 130 ambapo katika utambuzi na uendelezaji wa bunifu hizo wanashirikiana na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia(COSTECH)”amesema Prof.Mdoe.
Amefafanua kuwa kutokana na utendaji dhabiti wa serikali mafaniko mengi yamepatikana ‘katika eneo la elimu ya ufundi na teknolojia ambapo katika mwaka wa fedha 2021 kiasi cha Sh. Bilioni 18 kimetengwa ili kujenga chuo kipya cha ufundi jijini Dodoma.
Amefafanua kuwa kutokana na utendaji dhabiti wa serikali mafaniko mengi yamepatikana katika eneo la elimu ya ufundi na teknolojia kwa upande wa ujenzi wa uchumi wa viwanda ambapo udahili katika vyuo vya ufundi umeongezeka kutoka wanafunzi 96,694 mwaka 2015 na kufikia 151,969 mwaka 2020.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho Dkt.Musa Chacha amebainisha kuwa wamewaandaa wahitimu hao kwa ajili ya kujumuika na jamii katika kutafuta maendeleo na kuleta mabadiliko nchini hivyo wakumbuke kuwa elimu na maarifa waliyopata ni mali ya umma.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Utawala wa Chuo hicho Prof. Siza Tumbo ameishukuru serikali kwa mchango wake katika kuboresha miundombinu ya chuo hicho kupitia fedha za mradi wa kukuza ujuzi na stadi za kazi.
No comments:
Post a Comment