HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 26, 2021

RITA yawataka wananchi kuandika Wosia

 


Na Mwandishi Wetu


WAKALA wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA)  umewataka wananchi kuendelea kujitokeza na kuandika Wosia ili kujiepusha na migogoro ya mirathi inayotokea mara kwa mara katika familia.

Hayo yalielezwa jana na Afisa Mawasiliano wa RITA Grace Kyasi katika viwanja vya Mnazi mmoja kunapoendelea maadhimisho  siku ya sheria nchini.

Grace alisema kuandika Wosia kuna  umuhimu wake huku akiwataka watanzania kuacha  mawazo potofu juu ya kuandika wosia ambapo alisema wengi wao wamekuwa wakiamini kufanya hivyo ni sawa na kujichulia kifo cha mapema  jambo ambalo halina ukweli.

Alisema kitendo cha kuandika Wosia  suala la kisheria na lenye faida kubwa  linapokuja suala la kusimamia Mirathi ya familia.

Pia RITA wamewataka wananchi kufika katika viwanja vya Mnazi mmoja kwa ajili ya kupata vyeti vya kuzaliwa kwa ambao hawana,kuandika wosia na masuala ya udhamini


Alisema vyeti vya kuzaliwa vina matumizi makubwa na ya umuhimu yakiwemo kusaidia kwenye masuala ya ajira,vitambulisho vya utaifa na hata mikopo vyuoni hasa kwa wanafunzi.

No comments:

Post a Comment

Pages