Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Pwani, Sadiki Nombo, akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kwa ajili ya kuzungumzia mambo mbalimbali yaliyofanyika katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita kuanzia mwezi Oktoba hadi Disemba mwaka jana.
VICTOR MASANGU, PWANI
UONGOZI wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU ) Mkoa wa Pwani umesema licha ya kuweka mikakati madhubuti ya kupambana na wimbi la rushwa lakini pia bado utaendelea kuunga mkono juhudi za serikali katika kuthibiti hali ya magonjwa mbali mbali ya milipuko kwa kuweka vitakasa mikono katika sehemu mbali mbali za kuingilia ila kila mmoja aweze kuzingatia suala zima la usafi pamoja na watumishi wake,
Hayo yamebainishwa na Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Pwani Sadiki Nombo, wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na masuala mbalimbali ya utekelezaji wa kazi zao ambazo wanazifanya pamoja na jinsi gani walivyojipanga katika kupambana na magonjwa mbali mbali ya milipuko.
“Kama ulivyoshuudia ndugu waandishi wa habari sisi bado tunazingatia sana maagizo ambayo yanatolewa na wataalamu wetu wa mambo ya afya na ndio maana mmeshuhudia katika kila sehemu ya kuingilia kuna vitakasa mikono pamoja na maji safi na salama kwa lengo la kuwawezesha watumishi wetu waweze kunawa mikono pamoja na wananchi wengine ambao tunawahudumia ili kuweza kuondoka na magonjwa ya mlipuko ambayo yanaweza kujitokeza,”alisema Naibu huyo.
Pia Nombo aliongeza kuwa kuna umuhimu mkubwa sana wa kuhakikisha watumishi na wananchi wanendelea kunawa mikono yao mara kwa mara na hii hali kwa asilimia kubwa kwa upande wetu itakuwa ni endelevu ili kuweza kuthibiti kabisa kuwepo kwa mlipuko wa magionjwa ambayo baadhi yake yanatokana na kutokunawa mikono ipasavyo.
“Kitu kikubwa kwa upande wangu ninachotaka kuwaomba watumishi wenzangu wote tuendeleaa na tabia ya unawaji mikono tena kwa kutumia vitakasa mikono pamoja na maji ambayo ni safi na salama na ndio maana tunahakikisha kila ifikapo asubuhi kuanzia pale geti kubwa la kuingilia tunaweza maji safi na salama pamoja na vitakasa mikono kwani hii itasaidia sana katika kujikinga na magonjwa hayo ya milipuko.”alibainisha Naibu huyo.
Katika hatua nyingine aliongeza kuwa serikali ya awamu ya tano lengo lake kubwa ni kuweka mipango kabambe ya kuboresha sekta ya afya hivyo na wao wataendelea kushirikiana na wataalamu mbali mbali wa afya ili waweze kufikisha ujumbe kwa watumishi na wananchi wa ameneo tofauti ambao wanakwenda kuhudumia katika ofisi zao juu ya umuhimu wa kunawa mikono kwa kutumia maji safi na salama.
No comments:
Post a Comment