HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 20, 2021

WASHINDI NMB MastaBATA WAJINYAKULIA MAMILIONI

 Meneja Mahusiano wa Idara ya Biashara na Kadi wa Benki ya NMB, Yusuph Achayo, akizungumza wakati wa kuchezesha droo ya Saba ya Promosheni ya Mastabata iliyochezeshwa jijini Dar es Salaam. kushoto ni Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha, Pendo Albert Mfuru na kulia ni ofisa huduma kwa wateja wa Benki ya NMB, Yvette Nkhoma.


Meneja Huduma za Kadi kwa Wateja wa Benki ya NMB, Yuette Lupilli akizungumza na mmoja wa washindi wa promosheni ya mastabata wakati wa kuchezesha droo ya saba iliyochezeshwa jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha, Pendo Albert Mfuru na katikati ni  Meneja Mahusiano wa Idara ya Biashara na Kadi wa Benki ya NMB, Yusuph Achayo.


Na Mwandishi Wetu

  

KIASI cha Shilingi Milioni 56.8 kimenyakuliwa na washindi kwa droo ya NMB MastaBATA, ikiwa ni fedha taslimu na bidhaa nyingine zinazoshindaniwa katika droo hiyo inayoendeshwa na Benki ya NMB.

Hadi jana jumla ya washindi 280 wa kila wiki wamepatikana ambapo kila mmoja alishinda Shilingi 100,000 fedha taslimu tangu kuanza kwake Novemba 2020.

NMB MastaBATA, ni Kampeni ya miezi mitatu iliyozinduliwa Novemba 24, 2020 na itadumu hadi Februari mwaka huu, ambako zawadi mbalimbali zinatolewa zikiwamo pesa, simu janja, jokofu, runinga na safari ya kwenda kupumzika Zanzibar, Serengeti na Ngorongoro.

Aidha, jana walipatikana washindi 40 wa kila wiki waliojinyakulisha Shilingi 100,000 kila mmoja, ambapo idadi ya washindi hao imefikia 280 katika Droo iliyosimamiwa na Pendo Albert, kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), ambapo kigezo cha ushiriki ni matumizi ya Kadi za NMB Mastercard na Masterpass QR.

Akizungumza kabla ya kufanyika kwa droo hiyo, Meneja Uhusiano wa Biashara ya Kadi ya NMB, Yusuph Achayo alisema jana ilikuwa ni droo ya saba iliyotoa zawadi za jumla ya Shilingi Milioni 4 ambapo ni Shilingi 100,000 kwa kila mshindi kwa washindi 40.

"Tumeshuhudia watu wengi wakijinyakulia zawadi mbalimbali ikiwemo fedha taslimu na vifaa vya nyumbani. Tunawashauri wateja wetu waendele kutumia kadi zao kwenye manunuzi na huduma nyingine za kifedha," alisema Achayo.

Aliongeza kuwa, ukiondoa droo za kila wiki, pia NMB MastaBATA imewazawadia jumla ya washindi 12 kati ya washindi 15 wa droo za kila mwezi ambao wao wamekuwa wakijishindia simu janja aina ya Samsung Galaxy Note20, yenye thamani ya Shilingi Milioni 2.4

"Wito wetu kwa wateja wa NMB wenye kadi za NMB Mastercard na Masterpass QR, kufanya manunuzi na malipo mbalimbali ili kujiwekea nafasi ya kushinda droo zijazo za kila wiki, kila mwezi na ile zawadi kuu ya Grand Finale," alisema Achayo.

Aidha, zawadi kuu ya Grand Finale ambayo ni utalii Zanzibar, Ngorongoro ama Serengeti, inawapa washindi uhuru wa kuchagua zawadi mbadala kama runinga iliyolipiwa DSTV miezi mitatu, Jokofu, Laptop, Simu (Samsung A70), Water Dispenser na Microwave.

Kwa upande wake, Pendo, Ofisa wa GBT, aliwataka wateja wa NMB kuendelea kutumia kadi zao ili kujishindia zawadi zinazotolewa na NMB MastaBATA, na kwamba mchakato wa kuwapata washindi unafanyika kwa kufuata sheria na taratibu.

No comments:

Post a Comment

Pages