NA ANDREW CHALE, CHALINZE
MBUNGE
Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha za ujenzi wa lambo kubwa kwa ajili
ya mifugo ndani ya Kijiji 6cha Chamakweza Kata ya Vigwaza katika
Halmashauri ya Chalinze, lililogharimu Tshs. Milioni 700.
Mbunge
amebainisha hayo jana 24 Februari wakati wa ziara maalum ya Naibu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul aliyetembelea kujionea lambo la
mifugo linalojengwa chini ya Wizara yake hiyo sambamba na kuangalia
miradi mingine ndani ya Halmashauri ya Chalinze.
Akimpongeza kwa hatua hiyo, Ridhiwani Kikwete alisema:
"Niendelee
kuishukuru Serikali kwa mambo makubwa na mazuri iliyotufanyia kwenye
eneo letu hili la Chamakweza na Halmashauri yetu ya Chalinze kwa ujumla.
Mhe
Naibu Waziri, katika bajeti ya miaka miwili iliyopita Serikali
ilituidhinishia kiasi cha fedha Tshs Milioni 700 kwa ajili ya ujezi wa
lambo hili." Alieleza Mbunge.
Mbunge aliongeza kuwa:
"Serikali
imeendelea kutoa fedha zingine ikiwemo Milioni 400 na nyingine Milioni
100 ikiwa ni sehemu ya kuimalisha afya na ustawi wa mifugo yetu katika
eneo ili la Chalinze.
Yapo
mambo mengi ambayo utayaona kwenye ziara yako leo. Lakini mimi
nimesimama nikikushuru wewe kwa niaba ya Serikali yetu, lakini kwa
upekee kabisa nimshukuru Rais wetu Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa
namna moja ama nyingine ameendelea kuangalia mifugo kama sehemu kubwa ya
vitu au njia inayoweza msaidia Mtanzania kujiondoa kwenye wingu la
umasikini.
Zipo njia
nyingi sana lakini kikubwa imekuwa ikichangia pato la Serikali kwa zaidi
ya asilimia 10 ambayo ni sehemu kubwa sana, kama mnavyofahamu sisi ni
nchi ya pili kwa idadi kubwa ya mifugo Afrika, tukiongozwa na wenzetu
Waethiopia." Alisema Mbunge.
Aidha,
Mbunge alimweleza Naibu Waziri huyo kuwa zipo changamoto mbalimbali
ambazo pia anaamini zitafanyiwa kazi kwani Serikali iliyopo madarakani
ni sikivu.
"Hapa
ulipokuja Kijiji cha Chamakweza ni sehemu sahihi kwani asilimia kubwa ni
wafugaji. Tunategemea utakuwa na msaada mkubwa sana kwetu sisi.
Niendelee tena kumshukuru Mhe. Rais kwa jinsi ambavyo endelea kuingalia
Chalinze na sisi Chalinze binafsi yetu tunamshukuru sana.
Mimi
na Mwenyekiti wangu na Baraza letu la Madiwani tunapokutana kwenye
vikao na kila siku hatuchoki kumuombea Mungu na aendelee kumpa nguvu,
kumuongeza hekma na maarifa zaidi iliaendelee kuiangalia Chalinze kama
sehemu ambayo inamuombea Mungu sana" Alimalizia Mbunge Mhe. Ridhiwani
Kikwete.
Kwa upande wake,
Naibu Waziri wa Mifugo na uvui Mhe. Pauline Gekul alibainisha kuwa,
Wizara yake oliamua kutoa fedha hizo ili kutekeleza mradi huo ambao
baada ya kukamilika utawanufaisha wananchi wa Chalinze hususani jamii ya
wafugaji iliopo katika kijiji hicho cha Chamakweza.
"Mradi
huu ulitakiwa kukamilika tarehe 28.02. 2021 na mkandarasi anaetekeleza
mradi akaomba muda wa wiki mbili hadi tarehe 10. 03. 2021 ili kumalizia
sehemu ya asilimia iliobaki. Hivyo basi nawaomba sana wafugaji kuzuia
mifugo yenu mbuzi, kondoo na ng'ombe kufika kwenye eneo la ujenzi kwa
sasa. Tunawaomba mvumilie kwa siku 14 kutopeleka mifugo kule ili
Mkandarasi afanye kazi zake kwa ubora amelize ndio patakuwa rasmi"
alisema Naibu Waziri Gekul.
Aidha Naibu waziri alitoa salam za shukrani kutoka kwa Mh. Rais Dk. Magufuli kwa wananchi wa Chalinze.
"Mhe.
Rais anawashukuru sana wananchi wa Chalinze ndio maana Serikali
imejipanga kuhakikisha wafugaji na wavuvi na wanannchi kwa ujumla
wananufaika na mapato yatokanayo na kodi zinazotolewa na watanzania kitu
kilichopelekea watenge bajeti kwa ajiri ya ujenzi wa bwawa hili la maji
kwa matumizi ya kawaida na kunyweshea mifugo hapa Chamakweza". Alieleza
Naibu waziri Gekul.
Aidha,
alimtaka Mkandarasi kufanya kazi kwa ufanisi na kuzingatia muda
aliopangiwa ili kukamilisha mradi huo kwa wakati huku pia kuona namna
atakavyoongeza idadi ya birika za kunywea mifugo pasipo kuathiri ubora
wa lambo hilo.
No comments:
Post a Comment