Baadhi ya washiriki mbalimbali kutoka makundi ya wanaume wa mabadiliko wakifuatilia majadiliano yenye lengo la kuwawezesha wanawake katika nafasi za uongozi Zanzibar, kushindwa kushika nafasi za uongozi katika uchaguzi mkuu uliopita 2020 hawapaswi kukata tamaa badala yake wanaombwa kuendelea kujijenga katika kushika nafasi hizo na nyengine katika uchaguzi ujao wa mwaka 2025.
Imelezwa kuwa licha ya wanawake wengi Zanzibar kushindwa kushika nafasi za uongozi katika Uchaguzi Mkuu uliopita 2020 lakini hawapaswi kukata tamaa badala yake wanaombwa kuendelea kujijenga katika kushika nafasi hizo na nyengine katika uchaguzi ujao wa mwaka 2025.
Kauli hio imetolewa na baadhi ya wanaume wa mabadiliko waliopatiwa mafunzo na Tamwa-Zanzibar chini ya ufadhili wa shirika la umoja wa mataifa lilojihusisha na haki za wanawake (UN Women) yenye lengo la kuwainua wanawake wa Zanzibar waweze kushiriki katika vyombo vya kutoa maamuzi mkutano uliofanyika ukumbi wa watu wenye ulamvau kikwajuni mjini Unguja.
Akitoa taarifa ya awali kutoka Mkoa wa Kaskazini Unguja Hassan Jani alisema baadhi ya watu bado kwenye jamii hawajatoa kipao mbele dhidi ya wanawake na uongozi na kwamba wanahitaji kubadilishwa ili waweze kutoa fursa zaidi na kuwaunga mkono wanawake.
Alisema licha ya kazi kubwa ya kuhamasisha wanawake kujitokeza kugombea katika uchaguzi uliopita lakini wanawake wengi wameshindwa kufikia malengo ya kuwa viongozi kutokana na sababu mbali mbali.
Akitaja baadhi ya sababu hizo ni pamoja na kutokuwepo kwa mshikamano kwenye jamii ambapo alieleza kuwa mshikamano ndio njia kuu ambayo ingeweza kuwainua wanawake wote waliogombea.
Akifafanua zaidi alisema suala la mshikamano na mani katika maeneo mbali mbali yatawezesha wanawake wengi kukubalika na kujengewa uwezo sambamba na kuendelea kuelimisha zaidi jamii kuona umuhimu wa kuwaunga mkono wanawake.
Katika hatua nyengine alisema wakati maeneo mengi yakiendelea kusubiri uteuzi wa masheha wapya wakuu wa mikoa wana wajibu wa kulitazama suala hilo pia na umuhimu wa ushiriki kwa wanawake katika uteuzi huo wa masheha wapya.
Pamoja na hayo alisema licha ya uwepo wa harakati za kuwawezesha wanawake katika nafasi za uongozi lakini bado baadhi ya wanajamii wana uelewa mdogo na kuhisi wanawake hawapaswi kuwa viongozi.
Wakati hayo yakijiri mshiriki mwengine kwenye majadiliano hayo Almas Mohamed Ally alisema kuna haja ya kutengeneza mazingira ya ushawishi katika ngazi za juu za chama badala kujengewa uelewa wananchi kwa kuwa vyama vya siasa navyo vina maamuzi yao kuwapitisha wagombea.
Sambamba na hayo alivitaka vyama vya siasa kuhakikisha nafasi za uteuzi kuwatazama zaidi wanawake ambao waliwahi kujitokeza kugombea licha ya kutofanikiwa kwao.
‘’Iwapo mazingira haya yatafanyika kupewa nafasi za uteuzi kwa wanawake waliogombea bila shaka idadi kubwa zaidi itaendelea kujitokeza wakiamini kuwa kugombea kwao hwenda ikawa fursa ya wao kupanda na kuwa viongozi’’aliongezea.
Kwa upande wake Ukhty Amina Salum Khalfan kutoka wizara ya elimu Zanzibar alisema Zanzibar kuna baadhi ya watu kwenye jamii wakiwemo viongozi wa dini wamendelea kuwa na mtazamamo wa kuwakandamiza zaidi wanawake na kuhisi hawapaswi kuwa viongozi.
Alisema hakuna sehemu yoyote hile katika vitabu vya dini iliokataza wanawaek kutokua viongozi badala yake imewekwa wazi kuwa wanawake wanapaswa kushirikishwa katika uongozi na kutoa maamuzi.
Pia Ukhty huyo alitoa wito kwa jamii kuacha mtazamo wenye lengo la kuwakandamiza wanawake wakidhani ni watu wanaopaswa kubaki ndani pekee wakati wanawake ndio wenye jukumu kubwa la ulinzi wa familia kazi ambayo hata wanaume wengi wanashidwa kuifanya.
No comments:
Post a Comment