WAZIRI
wa Madini Doto Biteko, akifungua Mkutano wa 7 wa Mawaziri wa nchi zinazozalisha madini ya Almasi Afrika
uliofanyika kwa njia ya Mtandao yani (Video Conference).
NA HAMIDA RAMADHANI, DODOMA
WAZIRI
wa Madini Doto Biteko amesema kuwa Kiswahili kimepitishwa kuwa moja ya
Lugha za Mawasiliano zitakazotumika katika Jumuiya ya nchi Zinazozalisha
Madini ya Almasi Afrika.
Kauli
hiyo imesemwa Aprili 8, mwaka huu na Waziri Biteko wakati akifunga
Mkutano wa 7 wa Mawaziri wa nchi zinazozalisha madini ya Almasi Afrika
uliofanyika kwa njia ya Mtandao yani (Video Conference) na kutanguliwa
na Mkutano wa Wataalam wa jumuiya hiyo ambapo Tanzania ilikuwa mwenyeji
wa mkutano huo.
Aidha,
Tanzania imekabidhiwa Uenyekiti wa Jumuiya hiyo nafasi ambayo itadumu
nayo kwa kipindi cha miaka 2 ikipokea kutoka kwa nchi ya Jamhuri ya
Namibia ambayo ilikuwa Mwenyekiti kwa muda wa mwaka mmoja.
Pia, nchi ya Zimbabwe imechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti na inatarajia kuwa mwenyeji wa mkutano wa 8.
Akieleza
kuhusu yaliyojadiliwa na kukubaliwa katika mkutano huo, Waziri Biteko
amesema kuwa mkutano huo umekubaliana kuwa kamati Tendaji ya Jumuiya
hiyo kufanyia kazi mapendekezo ya Maamuzi ya Mawaziri ndani ya kipindi
cha miezi sita na kutoa mrejesho.
Aidha,
Waziri Biteko ametumia fursa ya Uenyekiti wa jumuiya hiyo kuzisisitiza
nchi wanachama kutumia masoko ya madini yaliyoanzishwa maeneo
mbalimbali nchini, akilenga kuzifanya nchi wanachama kuyatumia masoko
hayo kufanya biashara ya madini .
Awali,
Waziri Biteko amewaeleza mawaziri walioshiriki mkutano huo kuhusu
mafanikio yaliyopatikana katika Sekta ya Madini kufuatia Marekebisho
yaliyofanywa kwenye Sheria ya madini ambayo pamoja na mambo mengine,
yalipelekea kuanzishwa kwa masoko ya madini katika mikoa mbalimbali
nchini ambapo hadi sasa, Tanzania ina jumla ya Masoko ya Madini 39 na
Vituo vya Ununuzi wa Madini 41.
Naye,
Waziri wa Madini na Nishati wa Jamhuri ya Namibia, Tom Alweendo wa nchi
ambayo imemaliza uenyekiti wake, ameitaka Jumuiya hiyo kupata viongozi
shupavu wa Kamati Tendaji watakaosaidia kuweka msukumo katika
utekelezaji wa malengo ya jumuiya hiyo.
Ameongeza
kuwa, kama wanachama ni lazima wachochee na kuweka mikakati ya
kupigania maslahi ya Afrika kwa madini ya Almasi ikiwemo kuzitaka nchi
hizo kuhakikisha zinalipa michango yao kwa mujibu wa sheria.
Pia,
Ametumia fursa hiyo kuelezea yale ambayo yalifanywa na nchi hiyo wakati
ikishikilia kiti cha Uenyekiti na kueleza kuwa, pamoja na kipindi chake
kukabiliwa na changamoto za janga la ugonjwa wa Corona, ilifanikiwa
kuunda kamati ya uendeshaji ya jumuiya hiyo.
Mkutano
wa 7 wa Mawaziri wa Nchi zinazozalisha madini ya Almasi Afrika,
umehudhuriwa na nchi zote 19 wanachama wa umoja huo zikiwemo Nchi za
Angola, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Afrika Kusini, Namibia,
Tanzania, Zimbabwe, Cameroon, Afrika ya Kati, Ghana, Togo, Guinea na
Sierra Leone.
Mbali na
hizo, Nchi waangalizi zilizoshiriki ni Algeria, Jamhuri ya Congo, Cote
D’ivore, Gabon, Liberia, Mali na Mauritania pia zimeshiriki.
No comments:
Post a Comment